Kumbukumbu ya Mfungo wa Ramadhani: Futari Nyumbani kwa Mayor Kitwana Kondo Oyster Bay na Upanga

Kumbukumbu ya Mfungo wa Ramadhani: Futari Nyumbani kwa Mayor Kitwana Kondo Oyster Bay na Upanga

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUMBUKUMBU ZA RAMADHANI: FUTARI NYUMBANI KWA MAYOR KITWANA SELEMANI KONDO OYSTER BAY NA UPANGA

Katika makala fikra zangu zinarudi nyuma miaka mingi sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama huu.

Wakati huo Mzee Kitwana Kondo alikuwa Mayor wa Dar-es-Salaam na akiishi Oyster Bay.

Mimi na wenzagu alikuwa kila ukifika mfungo atutualika futari nyumbani kwake na tutakuwa sisi na yeye peke yetu.

Akifanya hivi kila mwaka na hata alipokuwa si Mayor tena na kuhamia nyumbani kwake Upanga aliendelea kutualika nyumbani kwake kwa futari.

Mimi na wenzangu hawa tulikuwa vijana miaka hiyo.

Tulikuwa tukifika nyumbani kwa Mzee Kondo mapema kidogo na tutamkuta anatusubiri kavaa kanzu yake maridadi na kofia maridadi ya mkono.

Hizi kofia za mkono ni kofia zinazoshonwa na washoni mabingwa kwa mkono bila ya kutumia cherehani.

Kofia hizi bei yake huwa ghali lakini ukiitia kichwani utastarehe na nafsi yako.

Tulikuwa tunakwenda kwa Mzee Kondo na mapema kwa makusudi kwani tukijua bila ya mtu kutuambia kuwa sisi hatuendi pale kwa baba yetu kwa kufuturu na kuomba dua peke yake.

Tulikuwa tunakwenda kwa Mzee Kondo kuzungumza kwa utulivu kwani mfungo una kawaida ya kumpunguzia mja shughuli.

Hii hutoa utulivu na watu wakaweza kukaa kitako wakazungumza nafsi zikiwa zumetulia.

Mzee Kondo akituchukulia sisi kama wanae nasi tulimkiri kama baba.

Tukifika unakhisi khasa kuwa Mzee Kondo kafurahi kutuona.

Mzee Kondo hapa atatueleza mengi yaliyopita na mitihani aliyokutananayo binafsi na mengine aliyoona ndani na nje ya serikali kabla na baada ya uhuru.

Hakika mikasa mingi imepita.
Hila, njama na fitna ndani na nje ya serikali.

Ndani na nje ya TANU.
Nini sababu zake na kwa nini zilielekezwa huko zilikoelekezwa.

Wengine walishinda.
Wengine walizama hawakuweza kuogelea kufika ufukweni.

Mzee Kondo akikijua Kiingereza na fasihi yake.

Mzee Kondo akiwajua Waingereza na historia yao na mikasa mikubwa iliyowafika.

Mzee Kondo akimjua Cromwell na Becket.

Mzee Kondo akimjua Shakespeare na majambazi ndani ya kazi za Shakespeare.

Mzee Kondo atakuhadithia Richard The Third na roho yake mbaya na atakueleza tamaa ya kutawala ilivyomponza Macbeth.

Mzee Kondo alikuwa kahifadhi beti nyingi za Muyaka bin Haj na akikusomea utafurahi.

Haya Mzee Kondo hakuwa anatueleza "in abstract."

Ndani ya mazungumzo haya tuliweza kuwaona watu tuliowajua pamoja na hila zao.

Jua litazama pataadhiniwa tutafungua.
Tutasali kisha tutakaa mezani kufuturu.

Mazungumzo yataendelea.

Hapa Mzee Kondo atatuchekesha kwa mizaha myepesi ya shida ya mtu kuoa mke asiyejua kupika.

Hakika ilikuwa starehe.
"Haya fanyeni muondoke mkawahi tarwehe."

Mzee Kondo kaondoka duniani watu wengi hawajui uwezo wake mkubwa wa fikra.

Kilichonistaajabisha mimi ni kuwa aliweza kuwaaminisha watu wajinga wajione mbele yake wao wana akili kubwa kumshinda.

Hii ni sifa watu wachache mno wamejaaliwa.

Mpaka leo mimi najiuliza ni yale mafunzo aliyopitia ujanani katika vyombo vya usalama vya wakoloni Waingereza na Tanganyika huru chini ya TANU au ni hii hulka ya Waswahili kujishusha?

Kwani kwa hakika Mzee Kitwana Kondo alikuwa Mzaramo na Mswahili khasa.

Katika futari yake juu ya mapochopocho utakayokutananayo kuwa na uhakika hutokosa muhogo na papa.

Nahitimisha kwa kuweka shairi kipande kidogo kukidhi haja ambalo Mzee Kitwana Kondo alilopenda kulisoma ghibu:

''Akutendeae Mema,
Kushukuru ni lazima

Jaza ya mema ni mema,
Maovu kutoyatia

Mbona umeghafilika?
Kwa jambo lisilo shaka?

Shetani umemshika,
Na kumuacha Nabia?''

Mwenyezi Mungu mkunjulie baba yetu kaburi lake na lijaze nuru.

Amin.

1712114085079.png

1712114124974.png

1712114149612.png
 
Mzee wangu, i wapi picha mkipata futari pamoja na Mzee Kondo? Wallah nimesoma harakaharaka nipate kuiona kwa vile ndio utaratibu wako uliozoeleka kuambatanisha picha katika kumbukizi zako mujarab.
 
Umenikumbusha kesi yake na Martha Wejja aliyekua anafanya kazi RTD mshahara Mia tano na kumi (510) shs huku akigombea ubunge na gwiji mtoto wa mjini mla chapati.
Angalizo. Kama una makandokando yako, usipende kutatua matatizo yako mahakamani.
Kuna watu wanajua una chupi ngapi.
 
Hakika ni jambo jema kupata bahati ya kuwa karibu na watu wenye ufahamu wa masuala mbalimbali ya nchi yetu na jamii kwa ujumla.

Mungu awabariki wote ambao walishiriki kwa jasho na damu na kuifanikisha nchi yetu kuwa mahali ilipo sasa

Na kwa wote waliokuwa na hila na mipango binafsi ambayo kwa namna moja au nyingine ingehatarisha umoja na amani tuliyokuwa nayo na kuidumisha mpaka sasa awasamehe, na tutamshukuru daima kwa kutupigania kama taifa
 
Sh Mohamed,
Ahsante kwa kutuletea kumbukumbu mjarab, Muda umepita
Nina suali dogo lakini nategemea utalifafanua vizuri
Umesema Mzee Kitwana Kondo alikuwa Mzaramu na Mswahili hasa
Naomba utufafanulie Mswahili ni nani? Wengi wetu hatumjui nani Mswahili
Shukurani Sh Mohamed
 
Wandugu...
Kama ulimjua Kitwana Kondo basi mfano wake ndiyo huo wa Mswahili.
 
Picha ya kusindikizia uzi...kuna wengi hawakiwahi kumuona kitwana Kondo
 
Mzee wangu, i wapi picha mkipata futari pamoja na Mzee Kondo? Wallah nimesoma harakaharaka nipate kuiona kwa vile ndio utaratibu wako uliozoeleka kuambatanisha picha katika kumbukizi zako mujarab.
Nifah,
Sina picha tukifuturu.
Miaka ile ya 1995 hizi simu na camera ilikuwa bado lakini nimeweka picha utaziona.
 
Mzee wangu, i wapi picha mkipata futari pamoja na Mzee Kondo? Wallah nimesoma harakaharaka nipate kuiona kwa vile ndio utaratibu wako uliozoeleka kuambatanisha picha katika kumbukizi zako mujarab.
Kuna connection na ubuyu kule kwa kwa da Mange, vipi unasubiri mfungo uishe ndio ututumie connection na ubuyu humu? Chungu cha ngapi leo?
 
Hakika ni jambo jema kupata bahati ya kuwa karibu na watu wenye ufahamu wa masuala mbalimbali ya nchi yetu na jamii kwa ujumla.

Mungu awabariki wote ambao walishiriki kwa jasho na damu na kuifanikisha nchi yetu kuwa mahali ilipo sasa

Na kwa wote waliokuwa na hila na mipango binafsi ambayo kwa namna moja au nyingine ingehatarisha umoja na amani tuliyokuwa nayo na kuidumisha mpaka sasa awasamehe, na tutamshukuru daima kwa kutupigania kama taifa
Just...
Katika mazishi ya Mzee Kitwana Kondo niliombwa nizungumze.

Angalia hiyo video hapo chini na sikiliza maneno ya Hamza Mwapachu anayomweleza Abdul Sykes kuhusu umoja wa Watanganyika wakielekea kudai uhuru wa Tanganyika.

View: https://youtu.be/xx5uUO2BQkw
 
Alifariki lini vile nimeshasahau nahitaji kukumbushwa
 
Back
Top Bottom