Think2
JF-Expert Member
- Jan 3, 2025
- 3,087
- 6,024
Wakati tatizo la Uhaba wa Sukari linaibuka mwaka 2021 mwishoni, Serikali ilieleza kuwa linasababishwa na Viwanda kushindwa kusindika Miwa inayozalishwa nchini kutokana na udogo wa mitambo na uchache wa viwanda.
Hata hivyo, hali iliendelea kuwa mbaya na sababu zikaanza kutajwa kuwa ni changamoto za Mvua zilizochangia Miwa kuharibiwa ikiwa shambani. Likaibuka suala la utoaji Vibali kwa kampuni zitakazoingiza Sukari nchini ambapo aliyekuwa Waziri wa Kilimo Profesa Mkenda alisimama kidete kuwa Wizara haitatoa Vibali kwa kampuni ambazo sio Wazalishaji wa Sukari.
Baadaye Mkenda aliondolewa katika Wizara hiyo na baadaye Vibali vikaanza kutolewa kwampuni ambazo sio Wazalishaji wa Sukari ikiwemo kampuni ya ITEL ambayo usajili wake ulitajwa na Mbunge Luhaga Mpina kuwa ni kampuni ya kuuza Vifaa vys Kielektroniki zikiwemo Simu.
Hayo yote yamefanyika wakati wa uongozi wa Waziri Hussein Bashe chini ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Hii tanzania inahitaji ukombozi mkubwa wote waliohusika watiwe nguvuni wanamtandao wote wakiongozwa na boss wao SSH