jamani, machozi yananibubujika kwa fadhili hizo kuu za Mungu wetu. hakika jina la Bwana ni la kusifiwa sana.napenda niwashirikishe wimbo wa NITAMHIMIDI BWANA ulioimbwa na kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama. wimbo huu umetokana na Zaburi ya 34.
ni wimbo mzuri sana wa sifa na kwa habari ya mtu huyu, sikiliza kwa akini ubeti wake wa pili, hakika utabubujikwa na machozi jinsi Bwana anavyotenda ajabu na ishara nyingi, lol, asante sana Akili Kichwani kwa kumtukuza Mungu kupitia ushuhuda wa rafiki yako. ubarikiwe sana
wimbo: NITAMHIMIDI BWANA
kwaya: Uinjilisti Kijitonyama
Albam: sina hakika
1.
Nitamhimidi Bwana kila wakati,
sifa zake zi kinywani mwangu daima X 2
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
wanyenyekevu wasikie wakafurahi,
mwimbieni Bwana nyinyi pamoja nami,
na tuliadhiishe jina lake pamoja X 2
Kiitikio
Nalimtafuta Bwana akanijibu, milele
Akaniponya na hofu, Milele X2
Onjeni muone,
onjeni, ooh omjeni
onjeni muone, Bwana Yu mwema X2
2.
Nitamhimidi Bwana kila wakati,
sifa zake zi kinywani mwangu daima X 2
Masikini alimuita, Bwana akajibu,
Akamuokoa kwenye tabu, akawa huru,
malaika wa Bwana aja fanya kituo,
Kumzunguka kumuokoa,
Mtu wa Mungu X2
Nalimtafuta Bwana, milele ……………
Glory to God