Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUMBUKUMBUKU ZA ''THEORETICIAN'' KHAMIS ABDULLAH AMEIR ZIKO UWANJANI
Haya ndiyo maajabu makubwa katika historia za Afrika kuwa wanaostahili kupewa sifa hawasifiwi wala hawapewi medali sifa zinakwenda kwa wale Waingereza wanawaita, ''syncopaths.''
Hawa ni wale watu ambao bila aibu hata chembe watapinda migongo yao hadharani sa saba mchana hadharani wakainama kumfunga viatu muhisani wao.
Mifano iko mingi na watu hawa hawagusiki.
Wako juu ya sheria zote.
Hii ni fani maaluma ambayo kwa hakika na bahati nzuri ni watu wachache sana wanaiweza na kuimudu.
Lakini ni fani ya yenye manufaa makubwa sana inapodumu na wewe na halikadhalika ni fani yenye kubeba hatari nyingi inapokugeukia ikawa kibidu na kukupa mgongo.
Sikupatapo kumsikia Khamis Abdullah Ameir kabla mpaka siku moja Ahmed Rajab aliponiandikia kuhusu kitabu cha Hashil Seif akanitajia jina lake na kunitahadharisha kuwa huyu mtu si mtu wa kawaida katika historia ya Zanzibar.
Ahmed Rajab akamtaja kwa sifa kubwa akamwita, ''Theoretician.''
Hakika nilishtuka na nikapigwa na mshangao.
Nimeshtuka kwa sababu namjua Ahmed Rajab si mtu wa kutupa maneno yake ovyo ovyo.
Nilipigwa na mshangao kwa kuwa nilijiuliza imekuwaje mtu muhimu kama huyu sijamsikia nusu karne ya mimi kusoma historia ya Zanzibar na propaganda zote za Mapinduzi Daima?
Nilikutana na Khamis ''Theoretician'' Abdullah Ameir katika ukumbi wa ZIRPP nilipoalikwa kuwasilisha kitabu cha Hashil Seif, ''Mimi, Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar.''
Niikwenda kumsalimu na mara moja nilitambua kuwa Khamis Abdullah Ameir ni aina ya wale watu ambao wapo lakini hawaonekani.
Yupo lakini huisikii sauti yake.
Hasemi lakini yuko wala huhisi kuwepo kwake.
Lakini yupo ila wewe humuoni.
Anasikiliza zaidi ya yeye kuzungumza.
Huisikii sauti yake.
Utamfahamu na kumtambua katika yale atakayofanya.
Tulisalimiana na nikamtia katika mazungumzo na kumuulza kama anaandika kumbukumbu zake.
Yeye ananisikiliza na tabasamu kubwa liko usoni kwake.
Nikamuomba tupige picha ya pamoja na nikamfahamisha picha hizi ni kwa ajili ya Maktaba yangu na akanikubalia.
Kuanzia pale nikataka kumjua huyu ''Theoretician,'' Khamis Abdullah Ameir.
Naam nilifurahi na nafsi yangu.
Alinifikisha London ya miaka ya 1950 kabla hata lile wimbi la ''Wind of Change,'' la Harold Macmillan halijajikusanya.
Hii ilikuwa London iliyokuwa inafukuta na joto la siasa za kujikombia na ukoloni.
Khamis Abdullah Ameir yuko London kijana mdogo wa Kizanzibari kajikuta yuko pamoja na vijana wengine kutoka nyumbani Zanzibar na nchi nyingine za Afrika ya Mashariki, vijana ambao watakuja kuacha alama katika historia za ukombozi wa nchi zao kutoka katika ukoloni.
Vijana ambao wengine maisha yao yalikatika ndani ya nchi zao katika juhudi za ukombozi na wengine baadae.
Kwa kawaida vitabu vinavyoandikwa na wanamapinduzi huwa ''drab,''' nikiazima msamiati wa Kiingereza kutoka kwa mwalimu wangu Sheikh Mohamed Mlamali Adam, Allah amrehemu.
Yaani vitabu vinakosa mvuto kwa kukosa ya kuandika lakini mwandishi hakubali kuwa hana la kuandika ambalo halifahamiki.
Matokeo yake badala ya kuwa na kitabu kunakuwa na kabrasha la mkutano mkuu wa chama chake.
Mwandishi haelewi kuwa ili kitabu kiwe kitabu ni lazima kiwe na elimu mpya ambayo jamii haina.
Hii ni tofauti na vitabu vingine katika historia ya Zanzibar vilivyoandikwa na Wazanzibari wengine, ''removed,'' yaani waliombali na hawa kwa fikra.
Nina hakika Khamis ''Theoretician'' Abdullah Khamis anakuja na kitabu kitakacho tusomesha mengi tuliyokuwa hatuyajui hata kwa mbali sana.
Sijajua hiki kitabu hiki kiko duka gani nikitie mkononi.
PICHA:
Picha ya kwanza kitabu, picha ya pili kushoto Badawy Qullatein, Khams Abdullah Ameir, chini ni Hashil Seif na pica ya mwisho ni Khamis Abdullah Ameir na Mwandishi.