Kumbukumbu za Tewa Said Tewa Rais wa EAMWS Tanzania

Kumbukumbu za Tewa Said Tewa Rais wa EAMWS Tanzania

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUMBUKUMBU ZA TEWA SAID TEWA RAIS WA EAMWS TANZANIA
''Tewa, kesho tunakwenda kumpa huyu mtu, Nyerere, mamlaka ya kuendesha nchi hii. Kuanzia hapo, mara tu tutakapomchagua kutuongoza hakuna namna tena ya kumnyang'anya madaraka tuliyompa. Hatumfahamu vizuri sana lakini natumaini kila kitu kitakwenda sawa.''
(Abdulwahid Sykes 1953)

1698607436253.png

Siku moja Mzee Tewa Said Tewa aliniita nyumbani kwake akanipa faili hilo hapo juu akaniambia nikalisome kisha tuzungumze.

Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nilifanya mazungumzo na Mzee Tewa nyumbani kwake na kwa hakika nilikuwa sipugui kwake na nilipojua kuwa alikuwa anapenda nimtembelee na kufanya mazungumzo ikawa napita kwake kila nilipokuwa na wakati.

Nilijifunza mengi.
Mengine nimeyaeleza katika kitabu cha Abdul Sykes mengine bado.

Baadhi ya historia yake na yaliyotokea hadi EAMWS kupigwa marufuka na serikali yanatoka katika nyaraka nilizosoma katika faili hilo.

Mzee Tewa alinieleza pia maisha yake binafsi na vipi yaliathirika kwa kuwa kiongozi wa Waislam.

Alipofariki mwaka wa 1998 nilikuwa nje ya nchi.

Niliporejea nikapitia magazeti ya nyuma kuangalia kama kuna mtu kaandika taazia yake.

Hapakuwa na kitu.
Zuberi Mtemvu alikuwa amefariki kipindi hicho hicho.

Nikatazama kama kaandikiwa taazia.
Hapakuwa.

Nilinyanyua kalamu nikaandika taazia ya Tewa kisha nikaandika taazia ya Mtemvu.

In Shaa Allah nitakuwekeeni hapa taazia ya Mzee Tewa mpate kumfahamu vizuri.

1698607045966.jpeg

1698607236222.jpeg

1698607271870.jpeg

1698607338038.jpeg


 
Back
Top Bottom