View attachment 2410295
PICHANI ni Nduna Songea Mbano Luwafu, alipigwa picha hii muda mfupi kabla ya kunyongwa na wajerumani Machi mwaka 1906.Mashujaa wengine 66 wa Majimaji walinyongwa Februari 27,1906.
Songea Mbano alinyongwa pekee yake siku tatu baada ya wenzake 66 kunyongwa na kuzikwa katika kaburi la pamoja àmbalo lipo katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea. Hata hivyo Songea Mbano alizikwa katika kaburi la pekee yake.Inasadikika wajerumani walikata kichwa chake na kuondoka nacho na hapa wamezika kiwiliwili chake.