1. "Mrengo wa kushoto" na "Mrengo wa kulia"
Maneno mawili, kiufundi, au hata manne. yanatumika kila siku, kote ulimwenguni, kuelezea misimamo ya kisiasa. Lakini maana yao ya awali ilikuwa halisi badala ya kiitikadi, na inatokana na Mapinduzi ya Ufaransa mwaka 1789...
Mfalme alikuwa amepinduliwa, lakini katika siku za mwanzo za jamhuri wafuasi wake walikuwa bado wapo.
Katika Bunge la Kitaifa wafuasi wa ufalme waliketi kulia kwa Rais, na wanamapinduzi upande wa kushoto kwake.
Baada ya hapo maana zao husika zikaibuka.