Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kuna jambo moja la ajabu sana kuhusiana na uhifadhi wao nyaraka ndani ya medulla ya binadamu. Jambo hili lipo hata katika baadhi ya wanyama kama tembo japo kwa mtazamo tofauti kidogo. Hawa wanyama wana uhifadhi wa kumbukumbu wa kutisha mno.
Mfanyie jema au baya, Jambo hilo litakaa kwenye kumbukumbu zake miaka mingi mbeleni. Sasa kwa binadamu kuna baadhi ya kumbukumbu zisizotoka hata iweje na kwa sehemu kubwa huwa ni kumbukumbu za utotoni na sehemu ndogo ujanani.
Sehemu fulani nyumbani kijijini
Watu/mtu fulani nyumbani kijijini
Tukio fulani nyumbani kijijini
Ndoto fulani nyumbani kijijini nknk
Ni kumbukumbu zisizokoma na kila zinapokujia hukuletea hali fulani hivi
Fadhaa
Hamaniko
Furaha
Huzuni
Mshangao nk.
Matukio haya ya hizi kumbukumbu hayaji kama fikra za kawaida bali huuvamia ufahamu wako kwa sekunde kadhaa na kujikuta kama uko huko na kisha hutoweka kwa haraka na kukuachia tafakuri nyingi.
Ni katikati ya muda huu mchache
Tunaangalia lakini hatuoni
Tunaitwa lakini hatusikii
Tunasemeshwa lakini hatujibu.
Ni katikati hali hizi hizi ndio ajali nyingi hutokea na ni ajali ambazo hazina maelezo ya kueleweka. Ni kumbukumbu za ajabu kwenye ufahamu jadidi wa database ya uhifadhi wa nyaraka na matukio mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.
Cha kushangaza na kustaajabisha zaidi ni kwamba kuna matukio makubwa yanatutokea maishani mwetu lakini database zetu huyakataa kuyahifadhi.
Kwanini? Mwili wa binadamu ni zaidi ya tuujuavyo!