1. Tundu Lissu sio mtu mwenye kusema ukweli akausimamia.
Kwa kinywa chake anasema, mwaka 2007 aliandika waraka ulioitwa "list of shame" wakati huo akiwa na Dokta Slaa ukasomwa pale Mwembe Yanga.
Katika waraka ule Lowassa alitajwa kama fisadi papa (ashakum). Kwa wakati huo Lissu aliamini kuwa Lowassa ni fisadi asieweza kuvumilika. Ilipofika mwaka 2015 Lissu akashiriki kikao cha kumkabidhi Lowassa urais mtu alieaminika ni fisadi. Aghalabu, Dokta Slaa aliondoka kusimamia imani yake. Lissu akalamba matapishi yake!
Hapa ndio kusema kuwa, Lissu anaweza kusema jambo moja usiku halafu kesho akalikana kwa maslahi yake binafsi. Watanzania tunataka Rais mwenye msimamo, asie kigeugeu ambae yuko tayari kusimamia imani yake hadi mwisho. Dokta John Magufuli eneo hili amethibitisha kushinda. Msimamo wake dhidi ya korona ni ushahidi wa wazi. Tuchagulieni mtu huyu asimamie nchi hii kwa miaka mitano ijayo.
2. Tundu Lissu ni mtu muongo na msariti.
Kabla ya mwaka 2013 uhusiano kati ya Tundu Lissu na Zitto Kabwe ulikua mkubwa zaidi. Mmoja akiwa Naibu Katibu Mkuu Bara na mwingine akiwa Mwanasheria wa Chama. Wote walikua vijana wazuri wenye vission na Chama chao.
Ulipofika mwaka 2013, Zitto akautaka Uenyekiti wa Chadema, Lissu akabadilika, akamtengenezea Zitto kesi ya usariti wa Chama, akamfukuza Chama. Licha ya kuwa Lissu aliufahamu ukweli kuwa Zitto hakua na hatia isipokuwa aliponzwa na Uenyekiti lkn hakujali, akamsariti rafiki yake akaitangazia Dunia kuwa Zitto ni mtu hatari zaidi ktk siasa za upinzani. Akamchafua Zitto akanuka!
Tanzania tunamtaka Rais mwenye kusema ukweli hata kama unaumiza. Lissu alishindwa kusimamia ukweli kumtetea Zitto Kabwe kwa sababu ya maslahi yake kwa Freeman Mbowe. Huu ni udhaifu ambao mtu wa nafasi ya Urais hapaswi kuwa nao. John Magufuli eneo hili amefanikiwa sana, kwake black ni black na white ni white. Tuchagulieni tena mtu mwema huyu atufikishe 2025.
3. Lissu sio mtu mwenye kupenda Muungano.
Tangu zamani hata sasa amani ya nchi yetu imeshikiliwa na Muungano. Mwalimu Nyerere alipata kusema, tukikubali kubaguana kwa kigezo cha Uzanzibar na Ubara tukimaliza tutaanza kubaguana kwa kigezo cha Uchaga, Usukuma na Uzanaki. Alisema, dhambi ya ubaguzi haina mwisho, tunahitaji kuimarisha zaidi muungano wetu kuliko kuuvunja.
Tundu Lissu hapendi Muungano, msimamo wake na chama chake uko wazi. Amethibitisha hivyo Bungeni na ktk mahojiano mbalimbali. Tafuta mahojiano yake na Salama Jabir ktk kipindi cha Mkasi mwaka 2016. Kwa msimamo wake, hatufai kuwa Rais kwa sababu atauvunja Muungano wetu na huo ndio utakua mwanzo wa kufarakana.
Katika eneo hili la Muungano, John Magufuli na Chama chake amejipambanua wazi. Msimamo wake uko wazi kuwa atausimamia, ataulinda na kuuboresha zaidi kadili ya mahitaji na wakati. Tuchagulieni tena mtu huyu alitulize Taifa letu tuimarishe Muungano wetu kwa ajili ya umoja wetu, ushirikiano wetu na usalama wa Taifa letu.
4. Tundu Lissu si mtu Mzalendo kwa Taifa lake.
Ushahidi uko wazi kuwa Tundu Lissu sio mwaminifu na Mzalendo kwa Taifa lake. Kauli zake za kichonganishi dhidi ya Taifa lake, uhusiano wake na mataifa ya nje ni ushahidi wa wazi ktk eneo hili. Kuna wakati alitofautiana na Kiongozi wa ACT Wazalendo ktk msimamo wake wa kuisimanga nchi yake mbele ya wahisani pale aliposhauri Tanzania kunyimwa msaada kwa sababu za tofauti zetu ndani.
Kwa hoja hii Tundu Lissu anathamini zaidi mataifa ya nje kuliko Taifa lake. Hii ina maana moja kubwa kuwa anaweza kutumika wakati wowote kulihujumu Taifa lake endapo atakua na madaraka makubwa ktk nchi.
Tusimchague, hatufai ktk nafasi ya urais. Eneo hili John amedhihirisha mbele ya Dunia kuwa yeye kwake Tanzania iko mbele ya kila kitu. Hajakwenda kwao kuwapigia magoti kama Lissu, John na Tanzania, Tanzania na John. Tuchagulieni John kazi iendelee!!
5. Tundu Lissu si mtu mwenye busara na hekima.
Hekima ya mtu ipo ktk kinywa chake. Kama mtu hawezi ku-control kinywa chake hekima yake ni sifuri. Kinywa cha Lissu kinasema ulongo, kinatoa maneno ya kejeri, dhihaka na majivuno wakati wote. Lissu haheshimu mamlaka yoyote ktk nchi hii, kauli zake dhidi ya Rais wa Nchi ni ushahidi unaotesa nafsi za watu wema. Kauli zake dhidi ya Mahakama mara kwa mara na sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, ni ushahidi mwingine wa kijeuri unaoumiza nafsi za mamlaka.
Nafasi ya Urais wa nchi ni nafasi ya juu kabisa ktk nchi, ni nafasi inayopaswa kukaliwa na mtu mwenye busara na hekima za juu sana. Eneo hili John Magufuli amethibitisha pasina shaka kuwa hajambo. Mazungumzo yake na Viongozi wa dini na madhehebu, wafanya biashara na makundi mbalimbali ktk nchi ni ushahidi wa kujivunia. Tuchagulieni mtu huyu atusaidie kufika salama Ka'anani.
Nawasalimu; Kampeni za kistaarabu.com,
#MitanoTena!!
MenukaJr.