Kumekucha Afrika, haya Tanzania nao wanataka kuongeza miaka ya hatamu ya rais

Kumekucha Afrika, haya Tanzania nao wanataka kuongeza miaka ya hatamu ya rais

Mkuu hujasema kema kuwa jubilee wanabadilisha katiba mahakama isiwe na mamlaka ya kutengua wizi wa kura...

Kuna mengi sijayataja yanayotendeka kwenye nchi zetu hizi za Afrika, nimefanya kupitia juu tu, ila nikichimba zaidi hata mtasinzia mkiyasoma.
 
basi mkuu kama duniani kote hujui mataifa yenye awamu zaidi ya hizi nne za kwetu mjadala uishie hapa.
Sasa lengo lako ni kunipa mtihani au nikunipa hoja ili na mimi nikujibu?, Mimi nimezungumzia nchi za africa, bado sijaona nchi ya Africa yenye hizo term 20, kama hukuwa umeelewa hoja yangu pole sana, na karibu tena.
 
Binafsi sioni tatizo kwenye hili maadamu tu mchakato huu uhusishe watanzania wenyewe na maamuzi yatoke kwao
Uhuru wa kweli ni pamoja na wananchi wanavyoshiriki katika kuitengeneza katiba yao na hii kwa Afirika tu duniani kote ukomavu wa demokrasia unapimwa kwa vigezo hivyo
Kwahiyo kama watanzania tunadhani mabadiliko ya kuongeza muda kwa watawala wetu madarakani ni jambo zuri basi na tufanye
Hakuna awaye yeyote atakayedhani au kufikiri kwamba tunaminya demokrasia
Juzi tu waingereza wamejitoa kwenye jumuiya ya ulaya kupitia maamuzi ya kura ya wananchi
Sasa nini mbaya maamuzi hayo wakiyafanya wananchi?
Tuache ubwanyenye hakuna atakayefikiri kwa niaba yetu kama mnadhani tukirekebisha mambo yetu basi eti waafrika tuna matatizo
Hakunaga hiyo
Kwanza mauchaguzi ya kila baada ya miaka mitano yanatumalizia hela tu badala ya kujenga nchi tunabakia na masiasa uchwara ya akina furani
Ingelikuwa amri yangu basi ningepitisha awamu za uchaguzi ziwe kila baada ya miaka 20

Unalolisema linakaa sawa na limetulia kama mkimpata rais bora na mwenye uadilifu na pia uzalendo na uchungu wa nchi, ila inakuaje pale mkiwa na bahati mbaya ya kumchagua rais anayewakomoa na kuharibu, hivyo ina maana mtamvumilia miaka yote hiyo, sio?

Leo hii inawezekana mkawa na rais mumpendaye na anayetimiza, lakini kumbuka hamyajui ya kesho. Ipo siku atakuja dikteta na kukalia ndani ya miaka yote 14, mtasaga meno kwa vilio.
 
Uadilifu wake ni nini?
Jibu wewe maana ya uadilifu, toa vigezo unavyoona vinafaa rais avitimize ili aweze kuitwa muadilifu, halafu tuone kama Magufuli yumo ama hayumo, inawezekena neno muadilifu tukawa na uelewa tofauti kabisa
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Jibu wewe maana ya uadilifu, toa vigezo unavyoona vinafaa rais avitimize ili aweze kuitwa muadilifu, halafu tuone kama Magufuli yumo ama hayumo, inawezekena neno muadilifu tukawa na uelewa tofauti kabisa
Mnatakiwa mjibu ninyi mliomuita muadilifu..kumuita muadilifu haitoshi.orodhesha huo uadilifu wake.
 
Mnatakiwa mjibu ninyi mliomuita muadilifu..kumuita muadilifu haitoshi.orodhesha huo uadilifu wake.
Sisi katika vigezo vyetu ameweza kuvitimiza ndiyo sababu tumemtaja kuwa muadili, anayepenga ndiyo mwenye jukumu la kuthibitisha pingamizi lake, ukishindwa kuthibitisha ingia kwenye gari tuwe pamoja( If you can not fight them, join them)
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Sisi katika vigezo vyetu ameweza kuvitimiza ndiyo sababu tumemtaja kuwa muadili, anayepenga ndiyo mwenye jukumu la kuthibitisha pingamizi lake, ukishindwa kuthibitisha ingia kwenye gari tuwe pamoja( If you can not fight them, join them)
Unaruka ruka tu.bado haujajibu swali.labda nikuulize nitajie maendeleo kumi aliyoyaleta magufuli
 
Unaruka ruka tu.bado haujajibu swali.labda nikuulize nitajie maendeleo kumi aliyoyaleta magufuli
Kichwa chako kibovu kabisa, kuwa muadilifu na kuwa mchapa kazi ni vitu viwili tofauti, nilijua kwamba kichwa chako kimejaa makamasi na hujui unalotaka kuzungumza ndiyo nilikuambia mapema, toa vigezo vya uadilifu mapema ili tuwe kwenye uelewa mmoja, sasa unazungumzia achievements, unaweza ukawa umeleta maendeleo mengi tu na usiwe muadilifu. Huna hoja agiza beer na uendelee kulewa.
 
Kubadili viongozi hakujawahi iendeleza Africa, tatizo letu waAfrika tume kalili tu kubadili viongozi.. bora kuwa na kiongozi mmoja aliye mzalendo na kutawala miaka 40 kuliko kubadili kila term mafisadi wapya.

Africa viongozi ni wachache wengi wana tamaa za madaraka so akipatikana mtu anaonekana na amethibitisha ana nia njema na nchi bora aendelee kutawala...

Gadaffi alitawala Libya zaid ya miaka 40 lakini kenya sijui Nigeria sijui Namibia cjui TZ hatukuwahi kuwa na maendeleo ya infrastructure na watu(socially/economically) hata robo ya Libya during Gadaffi era
 
Hii Afrika inazidi kuwa tamu, tumeamua kuwa na demokrasia yetu wenyewe, kubadilisha gia angani ndio zetu.
Kagame alishabadilisha na kuhakikisha anatawala hadi achoke, Museveni juzi kalianzisha kwamba yeye atawale hadi afie kwenye madaraka. Halafu yeye kawaida kama tumjuavyo huwa hatanii, kuna jamaa fulani anaitwa Besingye kule kwake ambaye kawaida lazima apokee kichapo kwenye kila zoezi la uchaguzi mkuu.
Kuna yule Nkuruziza (jina hunipa matatizo) wa Burundi, kwake huwa hata simuelewi, keshajihakikishia ndiye pekee yake.

Wabongo nao wameibuka na kuhakikisha hawajaachwa nyuma kwenye mabadiliko haya ya Afrika yetu tuipendayo, naona na wao wanapeleka hoja bungeni kuongeza hatamu ya rais kuwa miaka saba, hivyo rais mmoja anapiga misele miaka 14 kwenye awamu yake.

Kenya napo sipaelewi, tumekaa mkao usiojulikana kichwa kiko wapi na mkia umeishia wapi. Mahakama kuu imetoa maamuzi ya kubatilisha matokeo ya uchaguzi, tume imetangaza tarehe mpya ya lini tufanye uchaguzi, upinzani hawajaridhia na wameamua kila siku itakua vioja, ni mimbio ya kukimbizana na mapolisi na kupora na wameahidi kuhujumu uchaguzi hadi aondolewe jamaa fulani anaitwa Chiloba, hawataki kumsikia wala kumuona. Huyo jamaa naye akihojiwa haishi kutabasamu huku akiahidi kukomaa, kwamba yupo kwenye maandalizi ya uchaguzi na makelele yote haya hayamuhusu.


Afrika hoyeee


-------------------------------------------------------

The wave of electoral law changes sweeping across East Africa and meant to favour incumbents appears to be gathering speed in Tanzania.

Chemba MP Juma Nkamia is next month expected to table a motion before Parliament to extend presidential terms from five to seven years, as is the case in Rwanda.

The law amendment is widely seen as a testing ground in favour of extending President John Magufuli’s tenure. He is currently serving his first term.

A political showdown is looming, with the opposition Chadema MP John Heche planning to separately table in Parliament a counter private motion to reduce the presidential term to four years, as is the case in the US.

The outcome of the contest is expected to have a bearing on the country’s constitution review that has stalled since 2015.

Mr Nkamia’s move comes weeks after another MP Stephen Ngonyani said President Magufuli should rule for 20 years.

In July a politician from the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) Laurence Mabawa, started a social media campaign dubbed “Baki Magufuli” (Stay Magufuli) and said he would travel across the country to have President Magufuli’s tenure in office extended.

President Mwinyi

The seeds for the agitation to extend Magufuli’s appear to have been laid in April when a former President Ali Hassan Mwinyi said that a law allowing President Magufuli to extend his tenure in office for four terms should be considered. The former president said the incumbent needed this to continue installing discipline in the civil service and enhance access to healthcare.

“If it wasn’t for term limits, I would have suggested that Magufuli should be our president for eternity,” he said.

Two months later, a section of residents from Geita in northwestern Tanzania, where the president comes from called for amendments to the Constitution to allow him to serve for 20 years.

Opposition

The opposition Chadema party believes the president is behind the campaign that is gaining momentum but Dr Magufuli has repeatedly said at public rallies that he would respect the Constitution and step down after serving his two terms in office.

The opposition also sees the moves by ruling party legislators as part of an attempt to set the agenda for the stalled Constitution review that was abandoned in the run up to the October 2015 election that saw President Magufuli succeed Jakaya Kikwete.

“We will be surprised if the agenda is discussed in parliament because the discussion since 2012 has been a new Constitution, not extension of term limit. If the president hasn’t sent the MP to push for such an agenda, he should come out to resist such calls,” said Chadema’s director of protocol, communication, ideology and foreign affairs John Mrema.

Chadema fears the country could be plunged into political chaos if Mr Nkamia tables the motion as was witnessed in Uganda two weeks ago when a motion to remove presidential age limits was introduced in Parliament.

“Such calls are dangerous for national security. We don’t want to pursue the Uganda route but we want a new constitution that would set a precedent as that in Kenya when the Supreme Court invalidated President Uhuru Kenyatta’s win on August 8 over electoral malpractices,” said Mr Mrema.

However, the ruling Jubilee party in Kenya is pushing changes that would make it harder for a presidential election to be allowed on account of technicalities without due regard to the numbers the winning presidential candidate garnered.

READ: NRM says Besigye factor behind rush to pass Uganda's age limit Bill

ALSO READ: Is East Africa’s democracy now at a crossroads?


Magufuli caught up in MPs’ bids to change term limits



Acha kulinganisha Tanzania yetu na ujinga, mambo ya kubadilisha muda ili kumuongeza Raisi ni kawaida kujadiliwa Tanzania, karibia kila Raisi aliyepita ilikuwa hivyo kuanzia Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli, sema Magufuli inavuma kwa sababu ya wivu, wengi wanatuonea wivu ndani na nje ya Tanzania yetu, kwamba tuna Raisi ambaye anaijenga Tanzania yetu, na wanashindwa kwenye hila hoja wanahamia kwenye ujinga,wote ni wapiga dili na wezi wa Rasilimali zetu, chadema.

Isitoshe hata USA watu walikuwa wanasema Obama asingempisha Trump na kwamba angeongoza kwa emergency hii ni kawaida na hutokea kila mahali, Raisi Magufuli mwenyewe ameshasema kwamba hana hiyo nia na ndiyo muhimu!
 
Unaruka ruka tu.bado haujajibu swali.labda nikuulize nitajie maendeleo kumi aliyoyaleta magufuli
Yapo zaidi ya kumi, na uzi wake upo huku umeandikwa na REDEEMER
 
Africa hatuhitaji democracy bali viongozi waadilifu.
Itakugeukia , kuna siku. Lowasa, Sumayewangeliona umuhimu wa kuwa na katiba bora haya yasingeliwakuta. They were embraced by CCM favour wakasahau their main duty ya HAKI kwa wote.
 
Huyu Rais wa Tz ni rafiki mkubwa wa Kagame,Museveni na Nkurunziza
Does that tell you something
NB: Pia rafiki wa Odinga
Wakibugi kumoa railway ngoma inahamia kwao.
 
Mkuu,unamaanisha hata Mwenyekiti wako nimpigaji?
Tena huyu ndo hafai kabisa.ila akiongea mbele zawatu utadhani malaika nasikia ana hotel za kutosha kwao mwanza na miradi yake mingi ni RC wa Dar bashite ndio msimamizi wake na ndio maana wanapatana sana.
 
Back
Top Bottom