Kumekucha! Bifu la Watangazaji wa Shilawadu na RC Makonda lafikia patamu na limenoga sasa

Kumekucha! Bifu la Watangazaji wa Shilawadu na RC Makonda lafikia patamu na limenoga sasa

Kunuka ni uchafu tu,kama mtu anavaa sox za plastic na anavaa akiwa hajakausha miguu ni uchafu.
Na mdomoni kama hapigi mswaki vizuri,hasafishi ulimi au na meno kwa upande wa ndani.
Na kama pia hasafishi upande wa jui uliounga na pua unasemaje ni ugonjwa usiotibika?
Au kama mtu ameweka "tartar"kwenye meno yake kutokana na kutotumia mswaki sahihi kwa muda mrwfu,wakati tartar ni mabaki ya chakula,unasemaje ni ugonjwa wakati ni uchafu?
Dawa ni kuwa na mswaki sahihi na mara nyingi ni ile "HARD",asitumie "MEDIUM" wala "SOFT"
*NB AMUONE DENTIST KWANZA asafishwe meno na ashauriwe namna ya kupiga mswaki na aina ya mwaki(siyo brand,ni ugumu) kutokana na meno yake.
Huo ni.ushauri sahihi
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
bongo bwana!

Unaweza kuta hili bifu ndo lilikuwa bado linaendelea chini kwa chini
 
Napenda kweli kusoma nyuzi zako. Ila kikwazo ni hiyo style ya kuandika. Nashindwa kabisa kusoma. Macho yanatumia nguvuu Badili for me please🙏🙏🙏🙏🙏
 
Nasikia Ruge anaumwa so kakonda kinyama duh soudy ataokolewa na nani wakati boss wake mgonjwa kalazwa.
Wenye habari kamili muje.
 
Unamwambia ' Mtoto Mpendwa ' kuwa ananuka / anatema unadhani atakuacha hivi hivi? Hakuna Watu wenye ' Visasi ' vibaya na visivyoisha kama wa Kanda ya Ziwa. Naomba niishie hapa tafadhali.
kwahiyo " mutahaba " wame mpo poison " kweli "?
 
Wakiwa katika Kipindi chao ambacho kilikuwa mubashara kabisa Mtangazaji muongozaji wa Kipindi pendwa na Watanzania wengi hadi Mheshimiwa Rais wetu JPM aitwae Soud Brown amekuwa kila mara akifumba Fumbo huku akicheka mno na mwenzake Kwissa.

Ukiwaangalia zaidi utagundua kuwa kwa yale yaliyowatokea wiki mbili zilizopita utagundua kuwa Kipindi chao Kizima cha leo ni kama vile na wao wameamua kulipiza Kisasi kwa waliyofanyiwa na ' Mvamizi ' Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Christian Makonda.

Mtangazaji Soud Brown amekuwa kila mara akifumba fumbo moja hilo hilo huku akilinogesha na Kiitikio na Mistari iliyopo katika Wimbo maarufu wa Ney wa Mitego wa WAPO huku kila mara akimuuliza mwenzie kuwa ' Je mlango wetu umefungwa? '.

Fumbo lenyewe la Mtangazaji Soud Brown ambalo si Siri kuwa amelielekeza ' makusudically ' kabisa kwa ' adui ' yao na ' mvamizi ' wao Makonda ni kama lifuatalo nalinukuu " Hata wanaovua Viatu na Soksi zao zinanuka Wapo........unasema Wapo.......hata wanaonuka Midomo pia Wapo......unasema Wapo.....Oya Kwissa umefunga mlango lakini?...... Jamani hata wanaonuka miguu wakivua Viatu vyao Wapo.......unasema Wapo......hata wanaonuka Midomo sana Wapo......unasema Wapo......Kaka angalia umefunga lakini mlango? Walinzi wapo gado?

Sasa Kazi imeanza na naomba mlio karibu na hawa Watangazi akina Soud Brown na Kwissa mtusaidie kutuulizia kutoka Kwao kuwa huyo anayenuka Soksi na Miguu akivua Viatu ni nani? Halafu na huyo anayenuka mdomo pia ni nani?

Chokoza wote lakini kamwe usichokoze na kuanzisha vita na Waandishi wa Habari kwani wana mbinu nyingi za kukuchafua, kukumaliza na ikibidi hata kukudhalilisha. Pole sana ' mvamizi ' Mkuu wa Clouds nadhani sasa Vita baina yako na wao ndiyo imeanza na imefika patamu mno.

Kuna Watu wanajua mno kulipiza Visasi hasa kwa waliyofanyiwa au mateso ya kimanyanyaso waliyopata.

Nawasilisha.
mkuu unatumia window gani hii alignment inatupa shida kusoma
 
mkuu unatumia window gani hii alignment inatupa shida kusoma

Window 7 halafu naipenda ' Kishenzi ' Mkuu na wala sina mpango wa kuibadilisha kwani wapo ambao hawapati nayo shida kama siyo taabu.
 
Naona ameamua kulala nao mbele akina Soudy Brown kazi wanayo
Kweli Dunia rangi rangile...kutoka 'huwa napenda sana kusikiliza shilawadu' mpaka kuja kusoteshwa lupango na Jamaa kuwachunia.

Nina uhakika kabisa sasa hivi hata ukimpigia Jamaa simu atakuuliza 'ni kina nani hao..mimi sijawahi kuwasikia'
 
Back
Top Bottom