Kumekucha, hatimaye lango la mwisho limefunguliwa rasmi

Kumekucha, hatimaye lango la mwisho limefunguliwa rasmi

Walker Water

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2022
Posts
842
Reaction score
3,357
Natumaini wote ni wazima wadau wa huku.

Lengo la kuleta uzi huu kwenu ni kutoa taarifa ya furaha na kuwaamsha usingizini kuwa ule msimu wa mwisho wa dunia tayari umeshafunguliwa na lango lake lipo wazi. Tuanze, miaka 2000 iliyopita waliokuwepo walishuhudia lango la pili kutoka mwisho likifunguliwa. Lango lililokuwa likubwa sana lilipelekea mifumo yote ya dunia kubadilika kabisa ikiwemo kuporomoka kwa mataifa yenye nguvu, kuzalishwa kwa zana mpya za kilimo, kivita na hatimaye baadhi ya mataifa yasiyo tarajiwa kupata nguvu.

Lengo langu si kuelezea lango hilo lililopita maana mambo yatakuwa mengi sana. Mimi nataka ufahamu kuwa unaposoma uzi huu shukuru Mungu wako kwanza kwa kupata neema kubwa namna hii ya kushuhudia hili lango la mwisho kufunguliwa na hatimaye upo msimu mpya. Pia, kama ulikuwa na mpango wa kujiua nakuomba acha kwanza na kama unawasiwasi kuwa miaka yako ya kuishi hapa duniani inakaribia kuisha omba Mungu wako akuongezee japo miaka michache ili uone na kushuhudia yafuatayo;

Moja, nakutaarifu kuwa nchi zote tajiri na matajiri mmoja mmoja dunia nzima wametikiswa sana na bado wanatikiswa na lengo ni kuibuka kwa nchi mpya na watu wapya watakaokuwa matajiri katika msimu huu mpya. Hao watu na hizo nchi ni mimi na wewe na nchi yetu ya Tanzania kama tutapata watu wenye akili za kutambua majira na nyakati lazima tuwe "superpower".

Pili, katika msimu huu wa mwisho wa dunia tutashuhudia vita sana, njaa sana, ukame, ukosefu wa viongozi wenye maono, malalamiko sana, watu wengi kukata tamaa, nyumba za ibada zitajaa watu, nyumba za waganga wa kienyeji zitajaa watu na vyuo na mashuleni kujaa wanafunzi. Kwanini iwe hivi!? Ni kwa sababu huu ni msimu wa mwisho na hivyo mifumo yote ya mfumo wa zamani inaachwa kwa kushindwa kutatua matatizo ya huu msimu mpya wa dunia.

Yaani wote duniani tumerudishwa kituo "A" (mwanzo) ili tuanze wote safari ya huu msimu mpya, ndiyo hivyo kama ulikuwa hujui changamka sasa na nchi nayo ichangamke. Ukitaka kufeli na kuachwa katika msimu huu jaribu kutumia mbinu za zamani, hizo hazipo tena na ukitaka kufaulu kirahisi tumia mbinu mpya za huu msimu.

Ukitaka kuelewa vizuri tafuta habari ya Nuhu na ngarika usome. Kwa ufupi ni kuwa dunia nzima iliangamizwa kwa maji na akabakia Nuhu,mkewe na watoto wao watatu na wake za watoto wao tu. Baada ya maji kukauka Nuhu alitoka ndani ya safina na huku watu wake wote wakiwa wanamtegemea na kumsikiliza yeye. Sasa ndiyo tupo hapo leo (ndiyo kama tumetoka ndani ya safina wote) na watu wote wanakutegemea wewe!,pambana sasa uwasaidie maana lango lipo wazi.

Mwisho, tunapata hizo changamoto tu hapa mwanzoni wa lango ili kutulazimisha kutumia akili zetu vizuri na baada ya muda tutaishi maisha mazuri sana kwa faida ya watakaoweza kutumia akili zao vizuri za nyakati na majira. (Wao na nchi zao zitakuwa mabilionea wapya)
 
Nuhu wetu ni yupi? kama ni akili zetu kama ulivyoandika, basi mfano wako haufanani na wa Nuhu.

Umeandika huu ndio mwanzo mpya kama vile tumetoka kwenye Safina, sasa iweje sisi tutoke kwenye safina ikiwa bado hapa ulimwenguni kuna njaa, vita, na majnga mengine?
 
Haka ka paragraph ka mwisho kameshakudhihirisha,

""Mwisho, tunapata hizo changamoto tu hapa mwanzoni wa lango ili kutulazimisha kutumia akili zetu vizuri na baada ya muda tutaishi maisha mazuri sana kwa faida ya watakaoweza kutumia akili zao vizuri za nyakati na majira. (Wao na nchi zao zitakuwa mabilionea wapya)""

Chadema na vibweka vyenu vya ajabu ajabu..
 
Nuhu wetu ni yupi? kama ni akili zetu kama ulivyoandika, basi mfano wako haufanani na wa Nuhu.

Umeandika huu ndio mwanzo mpya kama vile tumetoka kwenye Safina, sasa iweje sisi tutoke kwenye safina ikiwa bado hapa ulimwenguni kuna njaa, vita, na majnga mengine?
Wote tupo kituo "A" mwazo,hivyo Nuhu ni yule atakayetumia akili vizuri na mwenye kutambua majira na nyakati na chakufanya katika majira haya,hata wewe unaweza kuwa. Hizo njaa,vita nk,ni changamoto za msimu mpya lazima ziwepo kwenye kila mwanzo ili kuchuja watu wenye nguvu na na binadamu bila kupata changamoto hawezi kutumia akili vizuri na kushtuka kuwa huu ni msimu mpya.
 
Back
Top Bottom