Kumekucha, hatimaye lango la mwisho limefunguliwa rasmi

Kumekucha, hatimaye lango la mwisho limefunguliwa rasmi

Inawezekana sana tu,inategemea na namna nchi zilivyojipanga na si lazima waje kuomba msaada wa kifedha huku,hata sisi kama nchi kujitegemea tu na kuishi maisha ya hali nzuri na watoto wetu itatutosha sana. Cha msingi nafasi hii ya dhahabu tusiichezee.
Em jazia nyama ueleweke vizuri
Umeweka code sana bado
 
Wadau napenda kukumbusha tu kuwa sijui ni mimi mwenyewe naona namna tunavyozidi kuachwa mbali tena katika mbio hizi zinazoendelea!,ila mpaka mwakani tena tutakuwa tumeona mengi zaidi na mshindi rasmi atatangazwa baada ya miaka mitatu toka sasa.Angalizo;Usitegemee deep st(wazee wa ndani sana) kwani kwenye hizi nyakati wamekuwa vipofu wote na wao wenyewe hawajui kinachoendelea!,Mi nipo deep state ya ulimwengu wa roho kwa kweli tunapambana haswa lakini bado mambo mazito mno!.
 
Uzi mkubwa sana,
Mzuri sana, unatafakarisha na kufikirisha.
Unatupa maamuzi ya wapi tusimamie
Wakati wa Nuu ilikuwa hivi hivi, Yule mzee alionekana mlevi hana maana, anaanzaje kujenga safina kwenye kijiji ambacho hakina mto wa bahari!?
Lkn mwisho wa siku wajuaji wale walijiona kuwa bado hawajui.
Hongera mtoa Mada
Unastahili 5 star [emoji93]
 
Nyongeza;Hili ndilo lango la msimu wa mwisho wa watu wema na waovu kuchanganyika,linalofuata soon litawatenga watu wema na waovu na hapo fujo yake itakuwa ya kutisha sana!.(naomba tuliache kwanza hilo tulipambanie hili).
Na hili ukipata wasaa lidadavue vyema tuwe na Nondo zote mkuu
 
Wadau napenda kukumbusha tu kuwa sijui ni mimi mwenyewe naona namna tunavyozidi kuachwa mbali tena katika mbio hizi zinazoendelea!,ila mpaka mwakani tena tutakuwa tumeona mengi zaidi na mshindi rasmi atatangazwa baada ya miaka mitatu toka sasa.Angalizo;Usitegemee deep st(wazee wa ndani sana) kwani kwenye hizi nyakati wamekuwa vipofu wote na wao wenyewe hawajui kinachoendelea!,Mi nipo deep state ya ulimwengu wa roho kwa kweli tunapambana haswa lakini bado mambo mazito mno!.
Yape nyama zaidi codes ziwe uncoded tupate madini.
 
Uzi mkubwa sana,
Mzuri sana, unatafakarisha na kufikirisha.
Unatupa maamuzi ya wapi tusimamie
Wakati wa Nuu ilikuwa hivi hivi, Yule mzee alionekana mlevi hana maana, anaanzaje kujenga safina kwenye kijiji ambacho hakina mto wa bahari!?
Lkn mwisho wa siku wajuaji wale walijiona kuwa bado hawajui.
Hongera mtoa Mada
Unastahili 5 star [emoji93]
Shukrani. Ni vigumu sana kueleweka kwa muda huu,lakini kadri siku zinavyozidi kusogea ndivyo mambo yazidi kujidhihirisha.
 
Na hili ukipata wasaa lidadavue vyema tuwe na Nondo zote mkuu
Sawa sawa,nitajitahidi maana tulianza vizuri hizi mbio ila kwa sasa naona viti viwili vikubwa vinagombana njiani. Nyakati hizi lazima mmoja avunjwe pembe ndipo na sisi "nyasi" tuone kwa haya macho yetu.
 
Natumaini wote ni wazima wadau wa huku.

Lengo la kuleta uzi huu kwenu ni kutoa taarifa ya furaha na kuwaamsha usingizini kuwa ule msimu wa mwisho wa dunia tayari umeshafunguliwa na lango lake lipo wazi. Tuanze, miaka 2000 iliyopita waliokuwepo walishuhudia lango la pili kutoka mwisho likifunguliwa. Lango lililokuwa likubwa sana lilipelekea mifumo yote ya dunia kubadilika kabisa ikiwemo kuporomoka kwa mataifa yenye nguvu, kuzalishwa kwa zana mpya za kilimo, kivita na hatimaye baadhi ya mataifa yasiyo tarajiwa kupata nguvu.

Lengo langu si kuelezea lango hilo lililopita maana mambo yatakuwa mengi sana. Mimi nataka ufahamu kuwa unaposoma uzi huu shukuru Mungu wako kwanza kwa kupata neema kubwa namna hii ya kushuhudia hili lango la mwisho kufunguliwa na hatimaye upo msimu mpya. Pia, kama ulikuwa na mpango wa kujiua nakuomba acha kwanza na kama unawasiwasi kuwa miaka yako ya kuishi hapa duniani inakaribia kuisha omba Mungu wako akuongezee japo miaka michache ili uone na kushuhudia yafuatayo;

Moja, nakutaarifu kuwa nchi zote tajiri na matajiri mmoja mmoja dunia nzima wametikiswa sana na bado wanatikiswa na lengo ni kuibuka kwa nchi mpya na watu wapya watakaokuwa matajiri katika msimu huu mpya. Hao watu na hizo nchi ni mimi na wewe na nchi yetu ya Tanzania kama tutapata watu wenye akili za kutambua majira na nyakati lazima tuwe "superpower".

Pili, katika msimu huu wa mwisho wa dunia tutashuhudia vita sana, njaa sana, ukame, ukosefu wa viongozi wenye maono, malalamiko sana, watu wengi kukata tamaa, nyumba za ibada zitajaa watu, nyumba za waganga wa kienyeji zitajaa watu na vyuo na mashuleni kujaa wanafunzi. Kwanini iwe hivi!? Ni kwa sababu huu ni msimu wa mwisho na hivyo mifumo yote ya mfumo wa zamani inaachwa kwa kushindwa kutatua matatizo ya huu msimu mpya wa dunia.

Yaani wote duniani tumerudishwa kituo "A" (mwanzo) ili tuanze wote safari ya huu msimu mpya, ndiyo hivyo kama ulikuwa hujui changamka sasa na nchi nayo ichangamke. Ukitaka kufeli na kuachwa katika msimu huu jaribu kutumia mbinu za zamani, hizo hazipo tena na ukitaka kufaulu kirahisi tumia mbinu mpya za huu msimu.

Ukitaka kuelewa vizuri tafuta habari ya Nuhu na ngarika usome. Kwa ufupi ni kuwa dunia nzima iliangamizwa kwa maji na akabakia Nuhu,mkewe na watoto wao watatu na wake za watoto wao tu. Baada ya maji kukauka Nuhu alitoka ndani ya safina na huku watu wake wote wakiwa wanamtegemea na kumsikiliza yeye. Sasa ndiyo tupo hapo leo (ndiyo kama tumetoka ndani ya safina wote) na watu wote wanakutegemea wewe!,pambana sasa uwasaidie maana lango lipo wazi.

Mwisho, tunapata hizo changamoto tu hapa mwanzoni wa lango ili kutulazimisha kutumia akili zetu vizuri na baada ya muda tutaishi maisha mazuri sana kwa faida ya watakaoweza kutumia akili zao vizuri za nyakati na majira. (Wao na nchi zao zitakuwa mabilionea wapya)
Angalia usije ukawapaisha wafuasi wako mbiguni kwa kuwafungia na kuwachoma moto.
 
Mwacha tuone panapo vuja , Good thing we are alive to witness this transformation.
 
Back
Top Bottom