Kumekucha jamani.....niseme nisiseme?

Nashindwa kuchangia sababu nashindwa kuelewa Genta amekusudia nini kwa uwasilishaji wa mtindo huu tata.
 
acha mbwembwee,achia info

Nimesema amshaneni wote na ikifika Saa 6 Kamili naachia hadharani kila kitu. Ni jambo ambalo litatikisa kidogo. Haya fanya upesi waamshe na Wenzio wote halafu waambie Members wote wa JF wawe online kuanzia sasa na kama una Marafiki zako hapo Nyumbani au Nduguzo na hawapo JF waambie wajiunge haraka sana tena muda huu huu ili wasikose ' Kitu ' cha uhakika ambacho nakwenda kukiweka hapo Saa 6 Kamili kama dakika 40 kutoka sasa. Nikiona wengi wenu bado hamjaamka na hampo online sikiweki hadharani. Nataka Members wa JF muwe macho na hata kama mnajiandaa ' Kubaiolojiana ' sasa subiri Kwanza hadi mpate ' Kitu ' cha uhakika ambacho nakishusha. Ama hakika leo ni leo!
 
Tunasubiri break news

Ni Breaking News Mkuu na siyo Break News. Nashukuru tu kwamba wenyewe Waingereza wenye lugha yao hawapo humu JF ila wangekuwepo kidogo wangetushangaa. Vuta subira tafadhali, kaoge kabisa na ujiandae ikifika Saa 6 Kamili usiku dakika 39 au 38 kutoka sasa naweka ' Kitu ' hadharani ila nataka kila Member amuamshe mwenzake na kama nikiona nyote hamjaamka siweki na nabaki nacho mwenyewe. Amshaneni haraka mkae mkao wa kula. Leo ni leo Mkuu!
 
Unatupa adhabu au
 
Hakuna jipya kwako,habari za siasa huwa ni muongo 100%....Labda huwa nakuelewa kwenye kuchambua matukio ambayo yameshatokea na kila mtu kaona ,apo ndio nakukubali.

Na kutia chumvi ya uvinza katika maelezo yako mengi.

Zaidi ya hapo hauna jipya la kutuambia tena kwa hiyo exclusive yako .....Nina imani utatuingiza chaka 100%
 
Mpaka saa sita siyo poa

Tena mkiniudhi nitasema mpaka Saa 7 usiku. au kama vipi sijui tufanye niiweke hiyo taarifa Saa 8 Kamili usiku Mkuu. Wewe unashaurije? au tufanye Saa 9 Kamili kabisa Mkuu ili nisubirie Kwanza Members wabaiolojiane huko Vitandani mwao na wakimaliza najua watakuwa wameshachoka hivyo Mimi nitawachangamsha kwa hii taarifa yangu.
 
Unatupa adhabu au

Kizuri hakiji bila kukisotea na ndiyo maana hata Waingereza wanasema no pain no gain Mkuu. Halafu kama labda unaona adhabu si vibaya ukaachana nayo tu na ukaendelea na ratiba zako na maisha yako kwani sijamlazimisha Mtu anisubirie. Tena mkinitibua ndiyo naweza nisiseme kabisa. Mtu mwenyewe Mimi dakika mbili mbele. Yaani ni bora tu muwe wapole kuliko kunishinikiza mtakavyo nyie.
 
Huu ni uhuni,weka sasa hv tu kesho makazini ujue!
 
Poa
 
Reactions: Pep

Sasa kama kumbe unayajua haya yote kwanini tokea Saa 7 mchana nilipouanzisha huu uzi kila mara ulikuwa unaukodolea kuona kama nimeshaweka ' Kitu ' hadharani? Kwahiyo tuseme kwamba na Wewe ulijitoa mhanga kuteseka na kuusubiria huu uzi kwa muda wote huo hadi hivi unaona umechoka kusubiri ndiyo umeamua kuhara na kutapika hivi?

Sasa ndiyo umeshanitibua na umewaponza Members wote waliokuwa wamejiandaa kusubiri hiyo taarifa yangu na nimeghairi siiweki na badala yake nakuomba Wewe sasa wawekee taarifa yako ambayo unaijua au unayo ili uwaridhishe. Jamani Members wa JF nimeghairi kuweka nilichokidhamiria na nawaombeni lawama zenu zote mpeni au zipelekeni kwa Member Kibundi wa getto kwani amenitibua.

Mkitaka niweke hicho ' Kitu ' hadharani mwambieni atengue Kauli yake na yote aliyoyaandika hapo juu na aniombe radhi ili hiyo Saa 6 Kamili ikifika kama nilivyoahidi niwawekeeni hiyo taarifa na kama asipoomba radhi atakuwa kawaponza nyote na sitowapeni hii taarifa ambayo nawaambieni ni nyeti na muhimu mno ambayo siyo ya kuikosa.
 
Mkuu, ujue tunaheshimiana. Na kama umetibuana na huyo member Kibudu sisi haituhusu.
Nahesabu dakika zilizobaki 14 tu hapa
 
Mkuu, ujue tunaheshimiana. Na kama umetibuana na huyo member Kibudu sisi haituhusu.
Nahesabu dakika zilizobaki 14 tu hapa

Mpaka aniombe radhi tena nampa sasa dakika tano ( 5 ) asipofanya hivyo naghairi na lawama zenu zote mpeni huyo Jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…