Kumekucha: kamati ya waamuzi (ZFF) yasema Simba ilipendelewa

Hii makosa ya marefa huwa ni makubwa Sana sijui kwann huwa hayapewi uzito unaostahili. Hivi kweli kamati inaweza ikasema uzito WA Kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu? Hivi wanajua kama Hilo Kosa ndio limesababisha Singida kutolewa? Unasemaje Kosa halina uzito?
Kwenye Afcon hakuna mwamuzi toka Tanzania bara wala Zanzibar
 
Hii makosa ya marefa huwa ni makubwa Sana sijui kwann huwa hayapewi uzito unaostahili. Hivi kweli kamati inaweza ikasema uzito WA Kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu? Hivi wanajua kama Hilo Kosa ndio limesababisha Singida kutolewa? Unasemaje Kosa halina uzito?
Inaleta aibu .... mfano Kwa lile la APR tayar limetuchafua
 
Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), imesema kuwa Mwamuzi Nasri Salum hakustahili kuipa Simba kona iliyoifanya ipate bao la kusawazisha, katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, wakati ikicheza na Singida Fountain Gate jana kwenye Uwanja wa Amaan.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Waziri Shekha amesema uamuzi wa kuipa Simba kona katika dakika za nyongeza, haukuwa sahihi na kwa mwamuzi huyo alifanya makosa, japo kamati hiyo haiwezi kumpa adhabu.

"Nilikwambia kwamba tutachunguza na tumekutana leo, tumebaini kwamba kulikuwa na makosa ya mwamuzi. Haikupaswa kuwa kona. Hakuna sehemu ambayo mpira ulichezwa na mchezaji wa Singida na kipa akaudakia nje, hivyo haikuwa sahihi kuwa kona,” amesema na kuongeza;

“Ni makosa ya kibinadamu na ndio kosa pekee tumeliona baada ya kupitia ripoti na marudio ila sehemu zingine zote alikuwaa sahihi. Uzito wa kosa alilofanya hautoshi kumpa adhabu refa huyo ukizingatia amekuwa akichezesha vyema mechi nyingi.”
UNa mambo ya kingese kweli
 
UNa mambo ya kingese kweli
Sio Mimi ni kamati ... Inasema mmebebwa
1704982251294.jpg
 
Sawa, wamerekebishe pia matokeo.
 
Hizo kamati za jecha Nani azihamini, mpaka leo hawajamwongelea maamuzi wa mechi ya mlandege na apr halafu wanatafuta umaarufu kupitia mgongo wa Simba .
Tukio la kubebwa Simba limeleta msisimko mkubwa zaidi
 
Back
Top Bottom