Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mgombea binafsi ni yule ambaye hatumii tiketi ya chama chochote ili kuweza kugombea nafasi ya kisiasa kama Urais na Ubunge. Kenya Walipitisha sheria hii March mwaka huu na wameidhinishwa wagombea Urais na ugavana bila kupitia chama chochote.
Wagombea 38 wameidhinishwa nafasi ya Rais nchini Kenya huku magavana 74 wakichonga nembo zao binafsi badala ya kutumia nembo za vyama vya siasa. Changamoto inayoonekana ni urefu wa orodha kwenye karatasi ya kupigia kura.
Nakumbuka wakili msomi, Mchungaji Mtikila enzi zake alitamba na hoja hii mpaka akafungua kesi ya kikatiba lakini bahati mbaya wazo lake liligonga mwamba mpaka anaaga dunia mwaka 2015 siku chache kabla ya uchaguzi.
Labda wabunge wetu wasipofungwa na vyama wanaweza kupata mawazo huru bungeni na kuwa na mgombea binafsi kwenye nafasi ya Urais kukabadili upepo hasa kwa wale wanaokatwa lala salama katika michakato ya vyama vyao. Pia inaweza kupunguza kugombania vyama kama kinachotokea NCCR na kule kwingine kambi mbili kuwa na vuguvugu kwenye chama kikongwe linalotarajiwa kuwa dhahiri 2025.
Hivi hili jambo lilikufa na Mtikila?