Tatizo sheria ya vyama vya siasa haisemi fulani akituhumiwa kwa wizi haruhusiwi kujiunga na chama cha siasa akipendacho..
Ndio maana nikaandika, ukituhumu, hakikisha una ushahidi wa kutosha, lakini sio kutoa tuhuma bila ushahidi.
Kule kusema msimamo wetu ni huu, hakuwezi kuwazuia wao kujiunga na chama chako wakiwa na madoa yao, hii tayari itaharibu taswira yako kwa jamii husika.
Vyama vya siasa havitegemewi kuwa na malaika. Uchafu wa mtu ni wake labda kama una baraka za chama chake.
"Vyama vya siasa vinategemewa tu kuwa na agenda za maana zenye kuwavutia watu."
Agenda zetu za wazi za kutaka usawa, haki na maisha bora kwa watu haziwezi kumvumilia mwizi bila kujali alipo.
Kwamba kuna rundo la mapesa lilishia China? Tunataka ushahidi upi kuwaaibisha wenye kuhusika? Labda kama tunadhani kuna majini yalifanya hilo?
Kwani waliozikusanya pesa hizo wanasema walizipeleka wapi au kwa nini walizipeleka huko? Kwa nini kuoneana aibu au kulindana hapa? Kila mmoja na akaubebe msalaba wake mwenyewe.
Kwamba hatujui mlolongo wa utunzaji wa pesa za serikali? Kwamba hata kikinuka kama hivi nani wanapaswa kuwajibika hatuwajui? Labda kama ni shamba la bibi.
Ushahidi upi tunaoutaka?
Kwani mzee Lowassa na akina Msabaha waliachia ngazi kwa ushahidi upi? Wengine si walisema walikuwa mbangusilo tu?
Au list Ile pendwa of shame ilituathiri sisi nini? Haikusaidia kuwawajibisha watu ile?
Wana tuingieni chimbo. Wote waliohusika kwenye hili wakapate kuanikwa peupe.
Hata kama Mbowe, Lissu, Samia, Mpango, Luoga, Dotto, Zitto, Rungwe, wewe, mimi nk walihusika na waanikwe tu!