Kumekucha Zahera amfukuza Cannavaro

Kumekucha Zahera amfukuza Cannavaro

Turnkey

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2013
Posts
7,359
Reaction score
5,837
KOCHA wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa yeye ndiye alimtimua meneja wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kuonekana kwenye ofisi ya Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji Mo licha ya yeye kufafanua kuwa alikuwa na ishu zake.

Lakini siyo hilo tu, Zahera amemhusisha staa huyo wa Zanzibar mwenye heshima Yanga na bao walilofungwa na Meddie Kagere kwenye mechi ya mwisho ya watani.

Cannavaro ambaye baada ya kustaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita alikabidhiwa cheo hicho, ametimuliwa na kocha huyo kwa madai kuwa anawasaliti na amekuwa na washikaji wengi sana wa Simba katika miezi ya hivi karibuni.

Zahera ameliambia Championi Jumatano kuwa, amefikia uamuzi wa kumtimua baada ya kufuatilia matendo yake kwa muda mrefu, lakini kubwa ni hilo la kuonekana kwenye ofisi ya bosi huyo wa Simba wakati Yanga ikiwa kwenye mapambano.

Mbali na sababu hiyo, pia Zahera anadai Cannavaro aliihujumu Yanga kabla ya kucheza na Simba Februari, mwaka huu na kufungwa bao 1-0 ambapo akiwa kama meneja, aliwaruhusu wachezaji kutoka usiku bila ya kocha kufahamu kitu chochote.

“Cannavaro hayupo kwa sababu alionekana katika ofisi ya bosi wa Simba anaingizwa mlango wa nyuma, watu walimuona, wakapigiwa simu viongozi wa Yanga kuambiwa kuwa Cannavaro, ameonekana akiingia katika ofisi ya bosi wa Simba, jioni alipoulizwa alisema kuwa alienda kumtafutia mke wake kazi.

“Lakini hili ni tukio la mara ya pili tulikua Morogoro kujiandaa na mechi ya Simba na siku mbili kabla ya mechi aliwaruhusu wachezaji watatu saa mbili na nusu usiku kwenda kukimbia mbio nje ya hoteli, waende hadi mjini bila ruhusa yangu.

Zahera aliongeza kuwa: “Kesho yake yule mtu wa ulinzi akaniambia kwamba Cannavaro aliruhusu wachezaji watatu kutoka usiku waenda kukimbia mbio, nikamuuliza walitoka dakika ngapi, mlinzi alisema hawakuchukua hata dakika 15 wakarudi.”

“Sasa siunaona kuna tatizo hapo nadhani siwezi kukubali mtu kama huyo katika benchi langu kutokana na mambo hayo,” alisema Zahera.

Hata hivyo, alipotafutwa Cannavaro simu yake haikupatikana huku ikidaiwa kuwa amekuwa akitumia simu ya ndugu yake kwa ajili ya kuwasiliana na watu wake wa karibu na hakuna ambaye tupo tayari kutoa namba hiyo.

Cannavaro ni mmoja kati ya wachezaji wa zamani wa Yanga ambapo alicheza kwa zaidi ya miaka kumi akiwa ametwaa makombe kadhaa makubwa.

CHANZO: CHAMPIONI
 
Yanga ni vile tu wana ukata ila nina amini wao wenyewe wameshamchoka zahera, huyu dingii ana vituko mnoo ni mtu wa kukurupuka mnoo ni km ze hedi of ze steti vile

Sasa goli la meddie limesababishwa na cannavaro alitaka nadir akakabe nadir ndio kipa azuie, nadir ndio aliyepiga kichwa kufunga ama anadhan ni PlayStation ile angempigisha nje!!
 
Zahera hawajui wachezaji wa Tanzania.
Hajui kuwa kuwa mchezaji wa Yanga au Simba ni wakati wa mechi tu.
Nje ya mechi hakuna uadui,
Unaweza ukamkuta mfadhiri wa Yanga akawa anawapa mshiko wachezaji flani wa Simba kwakuwa wamezoeana kwa muda mrefu.
Ni kawaida kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga wakawa wamezoeana sana na mfadhiri wa Simba MO kuliko hata wachezaji flani wa Simba na wakichacha wanaenda kumpiga mabomu ya pesa Cash na anawapa.
Hata wakati wa Manji kuna baadhi ya wachezaji wa Simba alikuwa anawapa mshiko kama kawaida hadi Ajibu akalowea na kihamia Yanga.
Kanavaro ni mchezaji wa muda mrefu hadi kwenye timu ya Taifa, hivyo lazima atakauwa anafahamiana vizier na MO ambaye hakosi katika kamati za kuihamasisha Taifa Star, hivyo sio jambo la ajabu kwa Kanavaro kwenda kwa MO kurekebisha mambo yanapoharibika.
Zahera kwake mpira ni uadui ndani na nje ya uwanja,
Ndio maana Yanga inapofungwa yeye ni kukasirika tu,
Na hawezi kuisifia timu pinzani kuwa imecheza vizuri.
Hata ilipofungwa na Simba aliishia kuwaponda wachezaji wake kuwa hawana akili.
Kila akifungwa lazima awalaumu TFF, Waamuzi na Timu ya Simba na kuwaponda wachezaji wake.
Kana kwamba Yanga haiwezi kufungwa katika mechi zake zote bila kuhujumiwa.
 
Hivi kiutaratibu anayetakiwa kumsimamisha mtumishi yeyote ndan ya klabu n nan maana naona Mwinyi anakila aina ya mamlaka ndan ya yanga mhazini ; msemaji meneja muajir na hata ukatbu mkuu naona kama anaichukua hii nafas ifke wakat wanayanga washtuke huyu mkongoman ana waingiza chakike
 
then mnategemea mpira watu upande Africa na Duniani kwa majungu kama haya!! ina maana Manara akikutana na Zahera hata wasisalimiane???
 
Nimeisoma hadi katikati hii taarifa kisha nikarudi mwanzo kabisa kwanza ili nijue kama ilikuwa ni ya tarehe 1 April nini!? Kucheki naona imepostiwa masaa 9 yalopita. Kama hayo yaloelezwa ni kweli basi Yanga tuna tatizo kubwa ambalo bado halijaleta matatizo makubwa na litaleta matatizo makubwa
 
KOCHA wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa yeye ndiye alimtimua meneja wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kuonekana kwenye ofisi ya Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji Mo licha ya yeye kufafanua kuwa alikuwa na ishu zake.

Lakini siyo hilo tu, Zahera amemhusisha staa huyo wa Zanzibar mwenye heshima Yanga na bao walilofungwa na Meddie Kagere kwenye mechi ya mwisho ya watani.

Cannavaro ambaye baada ya kustaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita alikabidhiwa cheo hicho, ametimuliwa na kocha huyo kwa madai kuwa anawasaliti na amekuwa na washikaji wengi sana wa Simba katika miezi ya hivi karibuni.

Zahera ameliambia Championi Jumatano kuwa, amefikia uamuzi wa kumtimua baada ya kufuatilia matendo yake kwa muda mrefu, lakini kubwa ni hilo la kuonekana kwenye ofisi ya bosi huyo wa Simba wakati Yanga ikiwa kwenye mapambano.

Mbali na sababu hiyo, pia Zahera anadai Cannavaro aliihujumu Yanga kabla ya kucheza na Simba Februari, mwaka huu na kufungwa bao 1-0 ambapo akiwa kama meneja, aliwaruhusu wachezaji kutoka usiku bila ya kocha kufahamu kitu chochote.

“Cannavaro hayupo kwa sababu alionekana katika ofisi ya bosi wa Simba anaingizwa mlango wa nyuma, watu walimuona, wakapigiwa simu viongozi wa Yanga kuambiwa kuwa Cannavaro, ameonekana akiingia katika ofisi ya bosi wa Simba, jioni alipoulizwa alisema kuwa alienda kumtafutia mke wake kazi.

“Lakini hili ni tukio la mara ya pili tulikua Morogoro kujiandaa na mechi ya Simba na siku mbili kabla ya mechi aliwaruhusu wachezaji watatu saa mbili na nusu usiku kwenda kukimbia mbio nje ya hoteli, waende hadi mjini bila ruhusa yangu.

Zahera aliongeza kuwa: “Kesho yake yule mtu wa ulinzi akaniambia kwamba Cannavaro aliruhusu wachezaji watatu kutoka usiku waenda kukimbia mbio, nikamuuliza walitoka dakika ngapi, mlinzi alisema hawakuchukua hata dakika 15 wakarudi.”

“Sasa siunaona kuna tatizo hapo nadhani siwezi kukubali mtu kama huyo katika benchi langu kutokana na mambo hayo,” alisema Zahera.

Hata hivyo, alipotafutwa Cannavaro simu yake haikupatikana huku ikidaiwa kuwa amekuwa akitumia simu ya ndugu yake kwa ajili ya kuwasiliana na watu wake wa karibu na hakuna ambaye tupo tayari kutoa namba hiyo.

Cannavaro ni mmoja kati ya wachezaji wa zamani wa Yanga ambapo alicheza kwa zaidi ya miaka kumi akiwa ametwaa makombe kadhaa makubwa.

CHANZO: CHAMPIONI
Champion gazeti la kipuuzi sana na machizi tu ndo wananunua gazeti kama hilo.
 
Nimeisoma hadi katikati hii taarifa kisha nikarudi mwanzo kabisa kwanza ili nijue kama ilikuwa ni ya tarehe 1 April nini!? Kucheki naona imepostiwa masaa 9 yalopita. Kama hayo yaloelezwa ni kweli basi Yanga tuna tatizo kubwa ambalo bado halijaleta matatizo makubwa na litaleta matatizo makubwa
Hamna ukweli wowote ni ujinga tu,Nadir anamuuguza mama yake Zenji
 
then mnategemea mpira watu upande Africa na Duniani kwa majungu kama haya!! ina maana Manara akikutana na Zahera hata wasisalimiane???
Mkapa alishawahi sema Waandishi wa Tz ni Wapumbavu, nawaandishi wa gazeti hili ni mojawapo
 
Yanga ni vile tu wana ukata ila nina amini wao wenyewe wameshamchoka zahera, huyu dingii ana vituko mnoo ni mtu wa kukurupuka mnoo ni km ze hedi of ze steti vile

Sasa goli la meddie limesababishwa na cannavaro alitaka nadir akakabe nadir ndio kipa azuie, nadir ndio aliyepiga kichwa kufunga ama anadhan ni PlayStation ile angempigisha nje!!
wakati said sued scud anaitungua simba mara mbili mwaka 1991..aliyeua anatengeneza mazingira na mipango ya simba kufungwa ni kiungo mahiri wa simba method mogella fundi...
 
Back
Top Bottom