A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na changamoto ya umeme katika mtaa wa Ipagala, Dodoma, kwa takribani miezi minane sasa. Tatizo hili hujitokeza zaidi nyakati za usiku, kuanzia saa moja hadi saa nne, hali inayowasababishia usumbufu na kuwanyima wakazi wa eneo hilo utulivu.
Licha ya kutoa taarifa kuhusu tatizo hilo, hakuna hatua za kuridhisha zilizochukuliwa hadi sasa. Badala yake, ofisi husika zimekuwa zikilaumiana na kutupiana mpira. Wakati mwingine, wahusika hufika kukagua tatizo na kutoa ahadi za kulitatua, lakini ahadi hizo hazitekelezwi.
Je, ni kwamba wakazi wa Ipagala hawana haki ya kupata huduma bora na ya uhakika ya umeme? Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka kutatua changamoto hii, ambayo imekuwa ikiathiri maisha ya wakazi kwa muda mrefu.