Kumekuwa na ongezeko la foleni kubwa jijini Dar es Salaam hivi sasa!

kadiri kasimba

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2022
Posts
588
Reaction score
1,150
Kumekuwa na ongezeko la foleni kubwa jijini Dar es Salaam, hasa kwenye barabara za kutoka Mwenge kwenda Tegeta, Mwenge kwenda Buguruni, na Posta kuelekea Mwenge, hasa nyakati za asubuhi na jioni.

Je, sababu ni magari kuongezeka? Au ni miundombinu ya barabara kuwa mibovu? Au ni kutokana na utengenezaji wa barabara za mwendokasi?

Maana kwa Dar es Salaam unaweza kupanga kufanya mishe sehemu nne au tano kwa siku, lakini ukaishia kwenda sehemu moja tu hadi jioni ikakukuta njiani. Kwa hali kama hii, maendeleo yanaweza kweli kwenda kwa kasi?

Nina ndugu yangu aliyetoka mkoa na kuja kunitembelea. Siku anaondoka aliniambia, “Huu mji mnauweza ninyi, mimi siwezi. Kuishi hapa hata nipewe bure, kila kitu foleni.”

Nini mtazamo wako kuhusu foleni zinazoendelea hapa Dar? Na nini kifanyike?
 
Dsm ni Kijiji kikubwa, siyo Jiji.

Majanga yote kabisa haya yamesababishwa na kukosekana kabisa kwa Mipango-miji.
Tanzania kuna Janga kubwa sana la kifo Cha Taaluma ya Mipango-miji.
Vijiji vyote kabisa nchi nzima ikiwemo na hicho Kijiji Cha Dsm hakuna Mipango-miji. Kila Kijiji kipo shaghala-bagala, hovyo hovyo, vururu-vururu kama vile mazizi ya ng'ombe
 
Kumekuwa na ongezeko la foleni kubwa jijini Dar es Salaam, hasa kwenye barabara za kutoka Mwenge kwenda Tegeta, Mwenge kwenda Buguruni, na Posta kuelekea Mwenge, hasa nyakati za asubuhi na jioni.

Je, sababu ni magari kuongezeka? Au ni miundombinu ya barabara kuwa mibovu? Au ni kutokana na utengenezaji wa barabara za mwendokasi?

Maana kwa Dar es Salaam unaweza kupanga kufanya mishe sehemu nne au tano kwa siku, lakini ukaishia kwenda sehemu moja tu hadi jioni ikakukuta njiani. Kwa hali kama hii, maendeleo yanaweza kweli kwenda kwa kasi?

Nina ndugu yangu aliyetoka mkoa na kuja kunitembelea. Siku anaondoka aliniambia, “Huu mji mnauweza ninyi, mimi siwezi. Kuishi hapa hata nipewe bure, kila kitu foleni.”

Nini mtazamo wako kuhusu foleni zinazoendelea hapa Dar? Na nini kifanyike?
Hata mimi kwakweli Dar kunaniboa sana,foleni kila mahali,ukisema uende kama kariakoo ndio balaa yani ni mwendo wa kugongana vikumbo tu,wacha tu niendelee kula raha huku village...
 
Back
Top Bottom