KERO Responded Kumekuwa na tatizo la umeme la muda mrefu katika eneo la Kimara Temboni - Arsenal

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Jumanne Mustapha

New Member
Joined
Dec 20, 2014
Posts
1
Reaction score
1
Wakazi wa Kimara Temboni, eneo la Arsenal, tunaomba kupaziwa sauti kuhusu tatizo la umeme linalotukabili kwa muda mrefu.

Transfoma iliyopo katika eneo hili ni ndogo na inahudumia zaidi ya kaya 250, hali inayosababisha kuzidiwa na matumizi na kusababisha umeme kukatika mara kwa mara, hasa nyakati za usiku.

Tumekuwa tukitoa taarifa mara kwa mara kwa TANESCO lakini hatujapatiwa mrejesho wa kueleweka. Tumekuwa tukipata hasara kutokana na kuungua kwa vifaa vya umeme, huku tatizo hilo likidumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Tunapoeleza changamoto hii kwa wahudumu wa dharura wa TANESCO tunaambiwa kuwa taarifa ipo kwa Meneja wa TANESCO Kimara, lakini hakuna hatua madhubuti iliyochukuliwa hadi sasa.

Tunaomba uongozi wa TANESCO Kimara kufanyia kazi suala hilo na kutoa suluhisho la kudumu ili wananchi tupate huduma ya umeme yenye uhakika.

MAJIBU YA TANESCO👇🏽​
 
Habari Jumanne Mustapha, asante kwa kuwasiliana nasi, na tunaomba radhi kwa changamoto hiyo.

Tumepokea taarifa yako, na wataalamu wetu watafika kabla ya siku ya Ijumaa kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kutatua changamoto hiyo.

Tafadhali tutumie namba yako ya mawasiliano kupitia ujumbe binafsi (Inbox) ili kurahisisha mawasiliano wakati wa utatuzi wa changamoto hiyo.

Asante.^FL
 
Habari ndugu mteja,
tafadhali tunaomba utupatie namba ya simu kwa msaada zaidi.^HN
 
Back
Top Bottom