Massy Planet
New Member
- Apr 14, 2024
- 1
- 5
Kutokana na tahadhari ya wataalamu wa hali ya hewa kuhusu uwezekano wa mvua kubwa za El Niño mwaka huu, tunaomba Serikali na mamlaka husika kuongeza juhudi za kutoa elimu na tahadhari kwa wananchi ili waweze kujiandaa mapema.
Pia, kuna wasiwasi kuhusu hali ya miundombinu ya mifereji ya maji, hasa katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo mitaro mingi imeziba na haijaondolewa uchafu. Endapo mvua kubwa zitanza bila maandalizi ya kutosha, kuna hatari ya mafuriko pamoja na kuongezeka kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Kwa mfano, katika maeneo mbalimbali ya Kinondoni, baadhi ya mifereji imeziba kiasi kwamba mvua ndogo tu husababisha maji machafu na hata maji kutoka kwenye vyoo kuingia barabarani na wakati mwingine kwenye makazi ya watu.
Tunaomba halmashauri na mamlaka zinazohusika zichukue hatua za haraka kusafisha mifereji, kutoa elimu kwa wananchi na kuweka mikakati ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza, badala ya kusubiri madhara yatokee ndipo hatua zichukuliwe.