Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

Kumfanyisha Interview Medical Doctor aliyethibitishwa na Baraza la Madaktari (MCT) ni dharau kubwa sana

Hivyo vyote sijui tabia, client care, humanity na vingine deep sana mpaka psychology ashavisoma na kafanya mitihani huko chuoni ya oral na written tena migumu ilioshiba, it doesn't make sense kwenda kumpima tena upya
Ivyo amevifanya chuoni na sio kwenye ajira sasa ni lazima wathibotishe kama anavyo kweli
 
Just imagine kijana kapata division one ya 7 au 10 form four kaenda high school kupiga PCB. Kapambana sana kachakaa kajitesa kajinyima kapata division one form six ya point tatu au tano.

Kaaply Muhimbili University kapitia mchujo katoboa akaanza masomo ya udaktari.

Kasoma miaka mitano bila kudisco tena kwa mateso makubwa bila kula bata mpaka kamaliza chuo.

Kabla hajaingia intern kafanyishwa mtihani wa MEDICAL COUNCIL OF TANGANYIKA katoboa kaanza interniship.

Kapiga intern kwa mwaka mmoja kisha kamaliza kisha kapigishwa pepa lingine la MCT katoboa.

Kasajiliwa na kutambulika kama MEDICAL DOCTOR na MCT.

Kijana huyu wa kitanzania aliyesoma kwa kujinyima na kujitesa tangu kidato cha kwanza leo hii anafanyishwa interview tena written interview sio prectical interview ili iweje?

Huyu kijana akikosa nafasi mnajua stress atakazopata mtaani na jamii inayomzunguka?

Hiyo michujo yote alopitia akipata ajira mnamlipa milioni moja na laki mbili ukitoa makato anabeba laki tisa bado mnampigisha interview ya nini sasa?

Hamuoni kama mnakatisha tamaa vijana waliopo shuleni na vyuoni?

Wadau

====================

UPDATES

Kwa taarifa nilizozipokea ni kwamba vijana wameitwq huko Galanos sekondali wakafanyiwe interview ya makaratasi

Hii nchi inashangaza sana
Hata sisi wakati tunajiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam miaka hiyo pamoja na kupata division one zetu kali kabisa kwenye kidato cha sita, bado tulifanyishwa mtihani wa kukubaliwa kujiunga na chuo uliofahamika kwa jina la matriculation!

Na kwa wale waliofeli huo mtihani; hata kama walipata division one; waliachwa! So wakati mwingine tujitahidi tu kubadilika kulingana na mazingira ya wakati huo.
 
Back
Top Bottom