Kumfukuza Malisa, CCM imepuliza ili Iwake, Hoja hujibiwa kwa Hoja , watu Sasa watazidi kuhoji kulikoni?

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Kuna vitu maamuzi yake huhitaji Hoja, yaan anasimama MTU makini anaelezea Kwa hoja !.

Sasa kumfukuza MTU namna hii, maana yake ni kuifanya habari iwe kuuuuuubwa , embu fikiria vyombo habari vireport " CCM yamfukuza aliyepinga kuvunjwa Kwa Katiba wakati wa zoezi za kuchagua Mgombea Urais'.

Habari kama hii Inakua Kubwa, inaamsha Hisia hata za waliolala , wanatambua kumbe Kuna uvunjifu wa Katiba uliofanyika?. Nao wao wanataman kujua ,wanafatilia zaidi na zaidi !!.

Maamuzi ya Busara ilikua ni Ama Kumpuuza, yaan Asijibiwe , au kumjibu tu Kwa hoja ili kuendelea kutoa sababu za kuhalalisha uhalali wa maamuzi ya Dodoma.

Sasa njia fupi ,Kwa mawazo mafupi , imekua ni Kusitisha Waandishi wa habari na kumfukuza Kwa kosa la Usaliti.

Khaaa yaan MTU kuhoji, ndio Usaliti?.

Kweli Kenge hasikii mpaka Damu imtoke masikioni.
 
Waliomtuma kupinga ndio waliompa urais huyo Mama!

Ogopa sana unapoona the so called watumishi wa mungu wanashauri jambo la kisiasa!!

Kadinal pengo alimshauri Membe amsamehe Musiba akakaza fuvu akawa yeye ndio Musiba na Musiba halisi anadunda!
 
Samia ni mwanamke katili sana
Unafikiri hayo yote anafanya yeye binafsi!!?ni hao TISS chawa wanamshauri Ili aharibu zaidi!unafikiri hata pale Dodoma siku Ile ni utashi wa mama!!?ni masterminder walimchezea mchezo Ili adore na kuchokwa mapema kabla hata kampeni hazijaanza!
 
Kuna vitu maamuzi yake huhitaji Hoja, yaan anasimama MTU makini anaelezea Kwa hoja !.

Sasa kumfukuza MTU namna hii, maana yake ni kuifanya habari iwe kuuuuuubwa , embu fikiria vyombo habari vireport " CCM yamfukuza aliyepinga kuvunjwa Kwa Katiba wakati wa zoezi za kuchagua Mgombea Urais'.

Habari kama hii Inakua Kubwa, inaamsha Hisia hata za waliolala , wanatambua kumbe Kuna uvunjifu wa Katiba uliofanyika?. Nao wao wanataman kujua ,wanafatilia zaidi na zaidi !!.

Maamuzi ya Busara ilikua ni Ama Kumpuuza, yaan Asijibiwe , au kumjibu tu Kwa hoja ili kuendelea kutoa sababu za kuhalalisha uhalali wa maamuzi ya Dodoma.

Sasa njia fupi ,Kwa mawazo mafupi , imekua ni Kusitisha Waandishi wa habari na kumfukuza Kwa kosa la Usaliti.

Khaaa yaan MTU kuhoji, ndio Usaliti?.

Kweli Kenge hasikii mpaka Damu imtoke masikioni.
Wamsikilize Mwl. J. K. Nyerere hapa.
 
Attachments

  • 5771391-6b7300c48c43013b94b420cc6e416c60.mp4
    8.3 MB
Utaratibu wa ccm ni rais kuhudumu vipindi viwili, hakuna mjadala zaidi kwa hilo!
 
Mkutano mkuu wa CCM ndo chombo cha mwisho cha maamuzi ndani ya CCM. Huyo kada kuanza kuhoji jambo lililopitishwa na mkutano mkuu ni usaliti na sio mwenzetu. Kufukuzwa ni halali yake.
 
Mkutano mkuu wa CCM ndo chombo cha mwisho cha maamuzi ndani ya CCM. Huyo kada kuanza kuhoji jambo lililopitishwa na mkutano mkuu ni usaliti na sio mwenzetu. Kufukuzwa ni halali yake

Maamuzi ya Mkutano Mkuu hayaruhusiwi kuvunja Katiba ya CCM!

Mkutano Mkuu hauwezi kuamua kuanzia leo mwanachama mwenye asili ya kisomali hawezi kugombea ukatibu, halafu tukasema wakiamua wameamua.

Kuna sheria zinazotawala utoaji maamuzi wa Mkutano Mkuu.

Sheria za Usajili wa Vyama, sheria za nchi, na Katiba yenyewe ya CCM.

Sheria za Nchi zinasema, kabla hujaanza kutumia mabadiliko ya katiba yako lazima Msajili apitishe!

Jakaya Kikwete wakati anatoa maagizo ya nini kifanyike alitamka kwamba HALMASHAURI KUU NENDENI MKAONDOE VIKWAZO VYA KISHERIA HALAFU MRUDI HAPA

Vikwazo gani ??????

Mwenezi Amos Makala akasimama akasema "haya, tunaendelea, meanwhile Alikiba, Zuchu, Mondi na Konde Boy jipangeni pandeni jukwaani wakati tunasubiri."

Wanaopaswa kubadilisha Katiba eti wamewekwa pembeni wakati taratibu zimeenda kuvunjwa pembeni huku tunapumbazwa na wasanii.

Ofisi ya Msajili ilikuwepo mkutanoni naamini - CHADEMA wao walitangaza "tuna ugeni Msajili yumo humu ndani jamani! "

Kwa nini ?

Kwa sababu Msajili yumo kushuhudia unafuataje katiba yako. Huwezi kuivunja kwa kusema nimeibadili leo leo! Ameipitisha kabla hujaitumia ?

Jakaya Kikwete aliposema Halmashauri Kuu nendeni pembeni "mkaondoe vikwazo," wakati Wachafu Media wanatusubirisha, Msajili alipitishwa kufutwa kwa vikwazo ???????
 
Kuna vitu maamuzi yake huhitaji Hoja, yaan anasimama MTU makini anaelezea Kwa hoja !.

Sasa kumfukuza MTU namna hii, maana yake ni kuifanya habari iwe kuuuuuubwa , embu fikiria vyombo habari vireport " CCM yamfukuza aliyepinga kuvunjwa Kwa Katiba wakati wa zoezi za kuchagua Mgombea Urais'.

Habari kama hii Inakua Kubwa, inaamsha Hisia hata za waliolala , wanatambua kumbe Kuna uvunjifu wa Katiba uliofanyika?. Nao wao wanataman kujua ,wanafatilia zaidi na zaidi !!.

Maamuzi ya Busara ilikua ni Ama Kumpuuza, yaan Asijibiwe , au kumjibu tu Kwa hoja ili kuendelea kutoa sababu za kuhalalisha uhalali wa maamuzi ya Dodoma.

Sasa njia fupi ,Kwa mawazo mafupi , imekua ni Kusitisha Waandishi wa habari na kumfukuza Kwa kosa la Usaliti.

Khaaa yaan MTU kuhoji, ndio Usaliti?.

Kweli Kenge hasikii mpaka Damu imtoke masikioni.
Akili hizo wazitoe wapi?
 
Mkutano mkuu wa CCM ndo chombo cha mwisho cha maamuzi ndani ya CCM. Huyo kada kuanza kuhoji jambo lililopitishwa na mkutano mkuu ni usaliti na sio mwenzetu. Kufukuzwa ni halali yake.
Ni chombo Cha mwisho kweli ,lakini ni Cha mwisho mara baada ya mchakato wa Ndani wa kikatiba kukamilika .
 
Back
Top Bottom