Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Jana nimekaa kilingeni na kuuliza mizimu ya babu wangu mzee Makunganya pale Kisarawe kama matokeo ya jana yalikuwa ya kimchezo kweli au mpira wetu unaelekea shimoni.
Kiukweli aliyonieleza na hata mm mwenyewe akili imekataa na haikubali kama Simba anaweza kufa mkono na Yanga. Mizimu inatoboa ukweli kuwa mkakati wa kuihujumu Simba ulipangwa uwe mchezo wa jana kwa sababu wahujumu waliamini kuwa ndiyo mchezo ambao wengi wataumia na utaleta mvurugano ndani ya timu.
Walipanga mipango bila viongozi kujua, waliwaeleza watu wa maadui zetu namna wanavoweza kuwasaidia kuimaliza Simba, mipango yao nje na ndani na kila kitu, hadi Rais wao akaenda kupanda mlima kilimanjaro ili kuishusha bendera na kibegi cha Simba wakaweka cha kwao, masharti yote aliyopewa injinia aliyafanya.
Watu wamechukua fedha za kutosha jana, Ali mradi tu mfadhili aachie timu, mwenyekiti aondolewe basi iwe tafrani tu na kwa sababu viongozi wetu wanapuuza taarifa zetu, wanatuona hatuna akili wao ndio wenye akili sana basi tumekaa tunawacheki tu.
Jana wengi hatukupata usingizi, yaani nimeshindwa kuelewa jana saa 8 tu usingizi umekata, kila nikiweka mawazo pengine mkono unanijia usoni.Usaliti ndani ya timu utaendelea mwanzo mwisho kwa sababu viongozi hawawekezi ktk kupata taaarifa, hawana watu wa mpira, jana hirizi zinawekwa laivu pale uwanjani na akina Moloko lakini nobody cares, watu wamefunguliwa geti lingine la kuingilia nobody cares.Nyie linganisheni doti tu, ceo wa zamani akadai Simba na mvua ni kama TMA halafu akacheeeeka kumbe alikuwa na maana yake na pale ndipo nilipogundua kuwa mambo hayatakuwa mazuri, asbh nilikuwa nimeandaa flame nyekundu, skafu nyekundu na kofta nyekundu lkn ilipofika saa 10 akili ilikataa kwenda uwanjani, sikuzivaa na nikaenda kuchek mtaani.Mizimu yake ilifanya kazi jana.
Ila no way, Al Qisas Haqu.