Kumfunga Simba bao 5 ni jambo ambalo haliwezekani na akili imekataa na kama ushindi ulikuwa halali bila kuhonga watu wetu basi nigongwe na gari nife

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Jana nimekaa kilingeni na kuuliza mizimu ya babu wangu mzee Makunganya pale Kisarawe kama matokeo ya jana yalikuwa ya kimchezo kweli au mpira wetu unaelekea shimoni.

Kiukweli aliyonieleza na hata mm mwenyewe akili imekataa na haikubali kama Simba anaweza kufa mkono na Yanga. Mizimu inatoboa ukweli kuwa mkakati wa kuihujumu Simba ulipangwa uwe mchezo wa jana kwa sababu wahujumu waliamini kuwa ndiyo mchezo ambao wengi wataumia na utaleta mvurugano ndani ya timu.

Walipanga mipango bila viongozi kujua, waliwaeleza watu wa maadui zetu namna wanavoweza kuwasaidia kuimaliza Simba, mipango yao nje na ndani na kila kitu, hadi Rais wao akaenda kupanda mlima kilimanjaro ili kuishusha bendera na kibegi cha Simba wakaweka cha kwao, masharti yote aliyopewa injinia aliyafanya.

Watu wamechukua fedha za kutosha jana, Ali mradi tu mfadhili aachie timu, mwenyekiti aondolewe basi iwe tafrani tu na kwa sababu viongozi wetu wanapuuza taarifa zetu, wanatuona hatuna akili wao ndio wenye akili sana basi tumekaa tunawacheki tu.

Jana wengi hatukupata usingizi, yaani nimeshindwa kuelewa jana saa 8 tu usingizi umekata, kila nikiweka mawazo pengine mkono unanijia usoni.Usaliti ndani ya timu utaendelea mwanzo mwisho kwa sababu viongozi hawawekezi ktk kupata taaarifa, hawana watu wa mpira, jana hirizi zinawekwa laivu pale uwanjani na akina Moloko lakini nobody cares, watu wamefunguliwa geti lingine la kuingilia nobody cares.Nyie linganisheni doti tu, ceo wa zamani akadai Simba na mvua ni kama TMA halafu akacheeeeka kumbe alikuwa na maana yake na pale ndipo nilipogundua kuwa mambo hayatakuwa mazuri, asbh nilikuwa nimeandaa flame nyekundu, skafu nyekundu na kofta nyekundu lkn ilipofika saa 10 akili ilikataa kwenda uwanjani, sikuzivaa na nikaenda kuchek mtaani.Mizimu yake ilifanya kazi jana.

Ila no way, Al Qisas Haqu.
 
Toka asubuhi kuna wachambuzi wanadai kuna dalili ya goli nyingi leo. Farhan na yule mzee wa jambia walisema hili.

Ni kama kuna mambo ya ndani waliyajua.
 
Mawazo kama haya ndio yanafanya timu yetu isifanye vizuri.

Mbona hao Yanga wakifungwa wanatafuta tatizo lilipo na kurekebisha? Sisi badala ya kutafuta tatizo TUNATENGENEZA tatizo.

Yanga iliyo bora kabisa imefungwa na Ihefu, kwa nini simba ikifungwa na Yanga ndio kila kitu kionekane kibovu?

Inamaana mnataka kutuaminisha kuwa, Simba ni timu teule Duniani ambayo haitegemei Kufungwa?

Ulaya kwenye Ligi bora ulimwenguni mtu anakula bao Saba sembuse ligi yetu changa?
 
Wakati wa kucheka cheka vizuri ukijua kuna wakati wa kilio. Kuna wakati tulicheka sana leo tunalia, kicheko kitakuja.
 
Goli 5 si chache. Waulize Yanga wamekaa muda gani tangu kupigwa goli 6 bila ndo utaelewa kwanini watu wana huzuni.
 
sisi wote tuliona ule mpira, tuambie, nani atakuwa alihongwa pale kati ya wale wachezaji wa simba? walionekana kujitahidi na kupambana ila walizidiwa maarifa, uwezo wa mtu mmoja mmoja, kila kitu. kwa kifupi timu yenu ni mbovu mbele ya yanga.
 
Yaani Kwa mpila ule waliocheza yanga Bado unawasiwasi na ushindi wa Gori tano? Yanga walistahili kabisaaaaaa! Simba walizidiwa kiufundi.
 
Mwenzako huyu
Your browser is not able to display this video.
 
we jinga na utagongwa
we jinga na utagongwa kweli, unashangaa nini Yanga ni timu ya 3 Afrika na ya 63 kwa ubora duniani. Angalia umeshakuwa mwehu mpaka unaongea na marehemu, Yanga ni habari nyingine we poyoyo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]

Makolo mtapata taabu sana

Hamsa [emoji113]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…