Kumiliki ardhi

Carina

Senior Member
Joined
Jan 4, 2011
Posts
194
Reaction score
70
Wakubwa,

Msaada kidogo,

Ninataka kununua tu eneo ambalo mtu ananiuzia, ninataka kujua nitahakikisha vipi kama hapa sipigwi na pia kujua kwamba hili eneo ana miliki kihalali. Eneo lenyewe lipo Kibaha

Ni vitu gani hasa vya kufanya kuhakikisha hapa kwamba sipigwi nanunua kihalali

Naombeni wataalam mnisaidie

Ni hayo tu naomba msaada.
 
Kwanza angalizo ukitaka kununua kiwanja mpe kazi mwanasheria lkn wewe mwenyewe huwezi ,wanasheria wanajua taratibu za mauziano za viwanja zaidi ya hapo utapigwa
 
kiuzoefu wangu,viwanja vingi vya kibongo havijapimwa na wengi tunanunua maeneo kienyeji,sanasana mwandikishiane serikali za mitaa,jaribu kuilizia majirani na kiwanja kama hakina shida au sio cha dhulma/mgogoro,,hati utafatilia mwenyewe baadae..
 
Kabla ya kufikia kuuziana fanya hivi;

Kama eneo limepimwa omba details zake, kama jina la block na namba ya kiwanja, then nenda kwa surveyor akuangalizie umiliki na kama kiwanja kina makando kando mengine au kiko clean, na je anayekuuzia kama ndiye mmiliki kama siye, yeye ni nani na anahusiana vipi na mmiliki.

Kama hakijapimwa hapo sifahamu wanahakikisha vipi kuwa haupigwi.
 
1. nenda idara ya ardhi kuhakikisha hakina miliki yoyote ya kisheria.... au matumizi yake ni yapi kama kiko kwenye planned area
2. Nenda serikali za mitaa na majirani wa kiwanja wanaweza kujua kama kina migogoro au la, then washirikishe katika kununua
 
Assnteni sana ssna kwa ushaurii nitaufanyia kazi
 
Kibaha patakuja kuwa Hot sana miaka ya baadaye .... kama kiwanja hakijapimwa jiridhishe serikali za mtaa kama ukikuta hakina changamoto yoyote chukua,
Kama kimepimwa mwambie akupe
Survey plan,
Ramani ya mipango mji

ili uende wizarani kujiridhisha na uhalali wa hicho kiwanja

Kibaha sio sehemu ya kuichukulia poa .Mwendokasi ushafika, Serikali ishaanza kuzungumzia mpango wa kutanua Barabara kuwa double road kutoka Kibaha to morogoro


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…