Kumiliki gari ni matatizo matupu

Ulimwengu wa Sasa yaani bado mtu unawaza umiliki gari Ili upate wanawake anyway KILA mtu na choice.
Ukingia tu kwenye page zao huko kwenye mitandao ukijitangaza unatoa huduma bure utakimbia mwenyewe. Nadhani lengo kuu la kuleta utandawazi ikiwemo ni kuharibu maadili ya jamii pia.
Zamani tulikunywa soda enzi za sikuu siku hizi pesa yako soda zipo tele mda wowote mahali popote tu ukitaka.
 
Hadi sasa kwenye uzi wako sijaona matatizo ya kumiliki gari ila naona matatizo ya umaskin ndo maana unalalamikia hadi mafuta sasa gari unataka itembee bila mafuta au service?

Mimi sina gari japo naamini kulinunua ninaweza nikijichanga ila kulihudumia sitaweza ndo maana sihitaji kwa sasa, sisi maskini wengi tukipata hela kidogo huwa tunawaza tu kununua gari ila hatuwazi Kama tunaweza kulihudumia na hapo ndo tatizo lilipo Hadi tunaaminishana gari ni tatizo lakin si kweli.
 
Sahii kabisa, uyu kipato chake hakiruhusu asitafute excuse TU[emoji4]
 
Sahii kabisa, uyu kipato chake hakiruhusu asitafute excuse TU[emoji4]
Ukiwa na kipato kidogo gari inakufilisi kweli siyo masihara.
Mi naona kwa sisi wenye vipato vidogo ni Bora tusikimbilie magari, kuliko kukimbilia kumiliki vitu vitakavyokua vinahitaji tutoe hela kila siku na Mara nyingine unatoa hela nyingi kuliko unacho kiingiza, ni Bora tu hiyo pesa ukaamua kujenga hata room 1 uokoe gharama za Kodi au ufanye biashara uliyo ifanyia utafiti kuwa itakulipa.

Wanasema kujenga ni uoga wa maisha.. NDIO ukiwa na kipato kidogo unatakiwa kweli uyaogope maisha na uheshimu pesa, kwa dunia ya sasa gari siyo anasa usafiri ni hitaji la muhimu lakin angalia Kwanza upoje kiuchumi je utalimudu?
 
True kabisa unless vijiwe vyako iwendako ni vya hadhi kiasi chake lakini otherwise ni kweli kabsa
 
Kama sio siku ya kazi si unatembea tu..ila kama ndio gari ya kwanza utataka uwe nayo muda wote hadi ukiwa unaenda kariakoo.
 
Ukinunua gari mbovu ndiyo utakutana na stress...

Ila hilo la kujitenga na jamii kuna asilimia za ukweli...
Cycle yako ya marafiki inakua ndogo sana...
 
Aisee wewe hutakiwi kumiliki chochote..

Kumiliki kazi ni stress.. Inabidi uamke mapema uwahi kazini..!
Kumiliki simu ni stress.. Inabidi umake sure ina charge na data ya kuja kupost JamiiForums..!
Kumiliki familia ni stress.. Inabidi uitunze..!
Kumiliki nyumba ni stress.. Inabidi ulipie kodi ya majengo..!
Kumiliki passport ni stress.. Inabidi kila baada ya muda fulani kuilipia upya..!

Hiyo ndio logic yako..!
 
Hata ukiwa na kipato Cha 2mil bado gari litakua changamoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…