Kumiliki laini zaidi ya moja ni ushamba uliokithiri

Sie tunaosafiri hapa na pale kwa mishe zetu tuna laini mitandao yote na zote ziko hewani. Simu mbili tu zinabeba laini sita. Kuna maeneo mtandao fulani haipatikani inabidi utumie mtandao unaopatikana eneo hilo
 
Unalaumu vitu usivyovijua. Sisi tunaosafiri mara kwa mara maeneo ya vijijini na tunahitaji network ili tufanye kazi unajua umuhimu wa kuwa na namba za simu zaidi ya moja. Nakupa mfano,
Ukiwa Morogoro maeneo ya Mvumi, Kilosa voda haifanyi kazi vizuri.....unashindwa kufungua kifile cha 20KB.

Ukiwa Mngeta meneo ya Mchombe na Ikule.....voda haishiki kabisa. Hata kupiga simu huwezi.

Ukiwa Malinyi maeneo ya Njiapanda Songea ndio kabisaaaaa, sio voda, halitel, airtel wala Yas. Kule ni TTCL labda,tena kwa Mbinde. Kuna siku niliteseka sana, mwenyeji wangu aliniacha mahali akaniambia yeye anatangulia lodge akanitajia jina.

Nilipohitaji kwenda lodge, nikasahau jina la lodge. Napiga simu hazitoki, yeye pia hanipati. Nimeita boda boda najaribu kumuuliza majina ya lodges lakini wapi.

Usilaumu mtu kuwa na namba zaidi ya moja. Kuna circumstances.
 
Nilicho gundya wewe ndiye mshamba
 
Kuna nyakati mtandao A huwa na shida, mtandao B utasaidia,kuna sehemu utakosa huduma kwa mtandao A mtandao C utasaidia, tatizo maisha yako yote ni kutoka mavurunza,panda mwendokasi nenda kkoo rudi
 
Ninazo za mitandao yote ila inayojulikana ni moja tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…