Kumiliki Nyumba mapema: Ndoto za Kiswahili au Presha ya Kizazi hiki?

Last_Joker

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2018
Posts
272
Reaction score
414
Siku hizi ukiwa kijana tu wa miaka 25 na huna hata kiwanja, basi tayari kuna watu watakutazama kwa jicho la “Upo nyuma mno bro/sis!” 😂 Hivi imekuwaje kumiliki nyumba imekuwa kama sehemu ya mashindano badala ya kuwa ndoto ya maisha ya mtu binafsi?

Zamani vs Sasa​

Enzi za mababu zetu, mtu akikazana sana, kajenga nyumba ya udongo baada ya miaka mingi ya kulima shamba au kuuza mazao. Ilikuwa kawaida mtu kumiliki nyumba akiwa na miaka 40 au zaidi. Hakukuwa na pressure, ilitosha kuwa na banda la kuku, mke na watoto wa kula ugali wa muhogo.

Sasa hivi? Bro, ukiingia TikTok tu kuna watu wa miaka 23 wanapost “My First Home Tour” huku nyumba ina tiles za kali kichizi na swimming pool ya mtoto wa mbwa. 😅 Na caption ni “Hard Work Pays” wakati sisi wengine bado tunaishi kwenye chumba cha kupanga cha self-contained kilichojaa harufu ya perfume, viatu na pilipili.

Je, Hali Inaturuhusu?​

Let’s be honest. Gharama za maisha ni kubwa mno. Rent, chakula, bando, presha za social media, ada za watoto (kama unazo), na bado unapaswa “u-invest.” Inakuaje mtu mwenye mshahara wa laki 6 anakuwa na pressure ya kujenga nyumba? Unless kuna miradi pembeni, mambo hayaendi tu!

Na hata ukitaka kujenga kidogo kidogo – bei ya viwanja, cement, mbao… ziko juu kuliko hata ndoto zako! Halafu bado kuna wale “wataalamu wa Instagram” watakukazia macho na kukuuliza, “Bro una miaka 30 bado unaishi na wapangaji wenzako?” Dah.

Presha ya ‘Soft Life’​

Kizazi chetu kimefungwa ndani ya picha ya ‘soft life’ – kila mtu anataka kuwa landlord, kusitiri familia, na kuwa na ka-garden kalikopandwa rosemary na mint ya kuweka kwenye chai. Lakini ukweli ni kwamba wengi wetu tunapambana, hatusemi.

Na kuna hili jingine – watu wanaona ukipanga ni hasara. “Bora jenge yako tu hata kwa matofali ya udongo.” Lakini si kila mtu yupo ready kisaikolojia, kifedha au hata kimipango kuingia kwenye project ya nyumba. Wengine bado wanajipanga, na hiyo ni sawa!

Hivyo Basi…​

Kumiliki nyumba si mashindano. Ni ndoto nzuri, lakini isiwe presha. Kila mtu ana wakati wake. Jenga taratibu. Usijichukie kwa sababu rafiki yako ana nyumba ya ghorofa Tabata au Mbweni – hujui aliipataje. Wewe endelea kupambana kwa njia zako.

Tujadiliane…​

Unaonaje hii presha ya “kumiliki nyumba mapema”? Ni motisha ya kizazi hiki au ni stress isiyo ya lazima?
 
Hautakiwi usikilize pressure toka kwa watu wa nje,jisikilize wewe mwenyewe,fanya ya kwako,ukifanya jambo kwa kusikiliza watu utapotea kimaisha,kuwa wewe na ujikubali.
 
Back
Top Bottom