Jana alijitokeza yule bush doctor kwenye vyombo vya habari akishambulia ufanisi duni wa bandari kama kigezo cha kumuuzia mwarabu na kwamba mapato yatokanayo na bandari ni pesa kidogo sana. Lakini huyu bush doctor ameshindwa kutambua kuwa tatizo la nchi hii siyo mapato bali ni ufisadi uliopindukia na matumizi holela ya pesa za umma.
Hii maana yake ni kwamba anataka kuathiri usalama wa nchi kiulinzi na kiuchumi akilenga kupata mapato makubwa yatokanayo na bandari ambayo kimsingi hayana msaada wowote kutokana na ubadhirifu na matumizi holela ya pesa za umma. Hayati Magufuli aliwahi kukiri kwamba nchi hii ina pesa nyingi sana hadi kuipa hadhi ya kuweza kuwa donor country.
Kwa hiyo point ya msingi iliyopo hapa ni kwamba bandari inamilikishwa kwa wageni jambo ambalo ni hatari kwenye usalama wa nchi na ulinzi wa rasilimali zetu yakiwemo madini na wanyamapori. Swala la ufanisi linaweza kufanyiwa kazi na TPA kwa ubia na kampuni za kitanzania au kampuni za nje lakini si kwa mkataba unaotoa umiliki wa bandari kwa wageni.
Nawasilisha.