Elections 2010 Kumkapenia Kikwete kwamgarimu Mwakyembe

Elections 2010 Kumkapenia Kikwete kwamgarimu Mwakyembe

kasyabone tall

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2009
Posts
254
Reaction score
63
Hotuba ya Dr, mwakyembe leo iliambatana na mbwembwe, matusi na dharau za kila aina, Lakini matusi yalizidi pale alipotaka wananchi wamchague kikwete na wananchi kupinga wazi wazi.

Alianza kumpigia debe Kikwete kwa kuwaeleza watu kuwa Kikwete anampango wa muda mrefu wa kuleta maendeleo Kyela, wananchi walipinga wazi wazi na akawaambia kuwa yeye alidhani anaongea na watu wenye akili, hakutegemea watu kupiga kelele za kupinga.

Hakuishia hapo akasema kama kuna mwanaume apite mbele ya mkutano na kisha wampigie simu Dr Slaa kwa pamoja halafu waone simu ya nani nitapokelewa. Hivyo yeye anamfahamu Dr Slaa na kusema hawezi kuwa na maendeleo kwa Kyela. Dr. Mwakyembe leo haliishiwa hoja kabisa.

Mkutano wake ulianza vizuri kwa kuleta stori za kupitisha jina lake ndani ya chama, na alimaliza huku akiacha watu wamechukia na wengine kuondoka pale alipomtetea kikwete na kutaka watu wamchague; upinzani alioupata ni somo kwake kuwa huyu mtu abebeki.

Watu wamemshauri ni bora ajipie kampeni yeye na mengine amwachie Kikwete mwenyewe.
 
DR. MWAKYEMBE AMESAHAU HAPA NDIPO CCM ILIPOBWAGA MANYANGAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

 
Last edited by a moderator:
Asipokuwa makini watamgeuka, hajui kuwa muungwana watu wamemchoka.
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka tu

ushawahi kusikia mtoto anakuwa kwa baba

jibu mnalo sio kosa lake;;;
 
JK alikuwepo mwenyewe Kyela na muda wote kushangiliwa. Iweje sasa eti wananchi wamechukia yeye kupigiwa kampeni?

Msaidieni mbunge wenu na wilaya yenu kusonga mbele na sio porojo kila siku. JK atashinda kwa kura nyingi Kyela.
 
JK alikuwepo mwenyewe Kyela na muda wote kushangiliwa. Iweje sasa eti wananchi wamechukia yeye kupigiwa kampeni?

Msaidieni mbunge wenu na wilaya yenu kusonga mbele na sio porojo kila siku. JK atashinda kwa kura nyingi Kyela.
.......Labda wamebadilika!
 
Siasa za MBEYA naona hazitabiliki, mie nathani wanasiasa waangalie lugha wanazotumia............
 
Mwakyembe anatetea kiti cha ubunge kwa tiketi ya CCM hivyo kumsifia bosi wake sio tatizo.Tanzania tunachagua wabunge kupitia vyama vya siasa sio mgombea binafsi,sasa mlitaka afanye je amsifu Dr Slaa?
 
Banyambala.jpgFaidini Ling'oma la Wanyakyusa
 
Huyu mwakyembe anawambia wanainchi kuwa JK anampango mrefu nao wakati hata akipita(Mungu aepushe) ana miaka 5. Aache ahadi general awe specific ni mipango ipi na itatekelezwa lini. Kama alizitaja ebu tuwekee hiyo mipango ya muda mrefu aliyonayo.
 
mwakyembe akileta mchezo naye hatutamrudisha bubgeni akitaka kutetea mafisadi
 
Huyu mwakyembe anajipendekeza nini? au anajifanya amesahau wana mtandao walivyotaka kumchakachua
 
Tatizo ccm wamechakachua siasa mpaka hazina maana,unaweza kuona watu wengi kumbe wamesombwa kutoka maeneo mbali2 na kugawiwa nguo,ile hali ya kwenda mkutanoni kwa utashi haipo,kwa sababu ya kuzoeshwa huu utaratibu wakisikia mgombea wa ccm atahutubia kitu cha kwanza wanauliza posho na usafiri vp?nachojiuli mbona mikutano ya dr slaa hawaulizi posho zaidi ya kutoa chochote kuchangia!,mtoto umleavyo.....au watu wameona hiyo ndo njia pekee ya kufaidi hela yao inayoibwa na serikali ya kifisadi ya jk na genge lake lisilo na huruma na uchumi wetu,ole wenu akishinda tena mjue kabla ya 2015 tutakuwa na noti ya 100.000.VOTE 4 CHANGE
 
Hivi jamani huko Kyela sio kule JK alikopondwa mawe miaka kadhaa iliyopita?
 
Mwakyembe mwakyembe . Ondoka huko ufisadini. Na udaktari wako huwezi soma alama za nyakati? Bure kabisa
 
Back
Top Bottom