MartinDavid
JF-Expert Member
- May 22, 2009
- 874
- 144
.
Mkuu.
Mbona unakuwa kama kasuku?
Upuuzi wa kusema Mkuu wa mkoa anahujumu maendeleo ya wilaya ni ujinga.Mbona Slaa kule mbulu alizungukwa kila upande,lakini alifanikiwa kwa kuwashawishi wafadhili wa ndani na nje ya nchi kusaidia?.Mbona kyela kuna watu wengi binafsi wanajitolea kutafuta wafadhili na kusaidia kwa manufaa ya wananchi wa kyela na Mbunge yeye ni kilio cha kusema anahujumiwa.
Mpesya( mbeya mjini),amezungukwa na wana mtandao,lakini hatujawahi kusikia anahujumiwa?
.
Upuuzi mtupu.
Unapochemka kubali na sio visingizo wa kubadili ID.
Kwann nibadili ID?.Ninakuogopa wewe?.
Binafsi sina muda wa kufanya Ligi na wewe.,mtu ambaye hakuna unalolijua kuhusu unachoaandika zaidi ya ngojera za magazeti kama ulivyosema mwenyewe.
Ilikuwa kila siasa za kyela zikiongelewa,basi swali enginneer kapotelea wapi.Sasa ni kila siasa za kyela afande samweli kapotelea wapi.Ndiyo ukasuku wenyewe huo ndugu yangu Keil.Ulikoelekeza ndiko hukohuko.Acha ukasuku.
Aliyeongoza zoezi la kumpa Ridhiwani heshima uchief ni Mwenyekiti wa zamani wa CCM Wilaya ya Kyela, Gracewell Mwakalukwa. Huyu hatokani na ukoo wa kitawala huko Kyela, ni kibaraka mkubwa wa Mwakipesile na hii yote ni kujikomba kwa JK. Kwa taarifa Dr Mwakyembe hajawahi shiriki hata mara moja katika matukio hayo kwa sababu watoaji huo uchief hawana sifa hiyo.
Pili Mwakipesile hajaathiri maendeleo ya Kyela tu bali mkoa mzima wa Mbeya. Mfano mmoja ni elimu, Quaresi ameiacha Mbeya ikiongoza katika mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi, leo hii tangu Mwakipesile apewe huo mkoa, Mbeya imeporomoka vibaya, inashika nafasi za kuanzia namba kumi na moja, lakini unamkuta mgombea bila aibu kwenye kura za maoni anawaomba wananchi wamchague kwa sababu anapatana na Mwakipesile!!!!
Kwa ufupi Mwakipesile na kundi lake wanaidhalilisha sana Kyela na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla na wamechangia kurudisha nyuma maendeleo mkoa huo.
Kwa ufupi Mwakipesile na kundi lake wanaidhalilisha sana Kyela na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla na wamechangia kurudisha nyuma maendeleo mkoa huo.