Aliyeongoza zoezi la kumpa Ridhiwani heshima uchief ni Mwenyekiti wa zamani wa CCM Wilaya ya Kyela, Gracewell Mwakalukwa. Huyu hatokani na ukoo wa kitawala huko Kyela, ni kibaraka mkubwa wa Mwakipesile na hii yote ni kujikomba kwa JK. Kwa taarifa Dr Mwakyembe hajawahi shiriki hata mara moja katika matukio hayo kwa sababu watoaji huo uchief hawana sifa hiyo.
Pili Mwakipesile hajaathiri maendeleo ya Kyela tu bali mkoa mzima wa Mbeya. Mfano mmoja ni elimu, Quaresi ameiacha Mbeya ikiongoza katika mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi, leo hii tangu Mwakipesile apewe huo mkoa, Mbeya imeporomoka vibaya, inashika nafasi za kuanzia namba kumi na moja, lakini unamkuta mgombea bila aibu kwenye kura za maoni anawaomba wananchi wamchague kwa sababu anapatana na Mwakipesile!!!!
Kwa ufupi Mwakipesile na kundi lake wanaidhalilisha sana Kyela na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla na wamechangia kurudisha nyuma maendeleo mkoa huo.