Kumkataa hakimu mfawidhi

Kumkataa hakimu mfawidhi

HPAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
410
Reaction score
567
Nauliza utaratibu ukoje ikiwa kwa sababu zenye mashiko, nimemkataa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo iliyo maeneo ya mjini. Hakimu naye amekubali kujitoa katika kesi hiyo lakini kwa kuwa yeye Mfawidhi (In charge/Kiongozi) wa mahakama hiyo amempangia Hakimu Mwingine aendelee kuisikiliza kesi hiyo ambaye kicheo ni mdogo.

Nataka kufahamu taratibu za kimahakama zinasemaje? Je haikuwa vyema kwa bosi huyo wa mahakama ya mwanzo kulipeleka jalada hilo katika mamlaka ya juu kiutendaji yaani mahakama ya wilaya ili iweze kuipangia kesi hiyo hakimu mwingine wa mahakama ya mwanzo ikiwezekana ikiwezekana hata kutoka mahakama ya mwanzo nyingine?

Kitendo cha Hakimu Mfawidhi mahakama ya Mwanzo kumpanga hakimu wa chaguo lake ambaye tena anaripoti kwake kinatia mashaka zaidi kama haki itatendeka, Naombeni ushauri wa kitaalamu kuhusiana na hili.
 
Hujaweka sababu ulizotumia kumkataa hakimu huyo, lakini kimsingi sababu zinazotakiwa ni kama hakimu huyo anaonekana kuwa na maslahi na kesi hiyo au ana uhusiano mbaya au mzuri na pande za walio kwenye kesi (mdai au mdaiwa/mlalamikaji na mjibu mashtaka)..

Kama amejitoa na kumpa hakimu mwingine ambae sababu zilizotajwa hapo juu hazimuangukii, huwezi kuomba ubadilishiwe hakimu. Mahakama ikiruhusu watu waombe kubadilishiwa mahakimu kwa sababu zozote tu, kesi hazitasikilizwa hata kidogo maana mahakimu watakuwa wanakataliwa sana.

Kimsingi, hapo hajakosea chochote huyo hakimu, pia hivyo vyeo vya kimadaraka sio vya muhimu sana kwenye kesi (hakimu mfawidhi nk) cha muhimu ni kuwa awe na sifa stahiki za kuhudumu mahakama hiyo basi..
 
Nauliza utaratibu ukoje ikiwa kwa sababu zenye mashiko, nimemkataa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo iliyo maeneo ya mjini. Hakimu naye amekubali kujitoa katika kesi hiyo lakini kwa kuwa yeye Mfawidhi (In charge/Kiongozi) wa mahakama hiyo amempangia Hakimu Mwingine aendelee kuisikiliza kesi hiyo ambaye kicheo ni mdogo.

Nataka kufahamu taratibu za kimahakama zinasemaje? Je haikuwa vyema kwa bosi huyo wa mahakama ya mwanzo kulipeleka jalada hilo katika mamlaka ya juu kiutendaji yaani mahakama ya wilaya ili iweze kuipangia kesi hiyo hakimu mwingine wa mahakama ya mwanzo ikiwezekana ikiwezekana hata kutoka mahakama ya mwanzo nyingine?

Kitendo cha Hakimu Mfawidhi mahakama ya Mwanzo kumpanga hakimu wa chaguo lake ambaye tena anaripoti kwake kinatia mashaka zaidi kama haki itatendeka, Naombeni ushauri wa kitaalamu kuhusiana na hili.
Jambo la maana Ni Hakimu afuate misingi ya sheria pasipo kuingiza utashi binafsi.
 
Back
Top Bottom