HPAUL
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 410
- 567
Nauliza utaratibu ukoje ikiwa kwa sababu zenye mashiko, nimemkataa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo iliyo maeneo ya mjini. Hakimu naye amekubali kujitoa katika kesi hiyo lakini kwa kuwa yeye Mfawidhi (In charge/Kiongozi) wa mahakama hiyo amempangia Hakimu Mwingine aendelee kuisikiliza kesi hiyo ambaye kicheo ni mdogo.
Nataka kufahamu taratibu za kimahakama zinasemaje? Je haikuwa vyema kwa bosi huyo wa mahakama ya mwanzo kulipeleka jalada hilo katika mamlaka ya juu kiutendaji yaani mahakama ya wilaya ili iweze kuipangia kesi hiyo hakimu mwingine wa mahakama ya mwanzo ikiwezekana ikiwezekana hata kutoka mahakama ya mwanzo nyingine?
Kitendo cha Hakimu Mfawidhi mahakama ya Mwanzo kumpanga hakimu wa chaguo lake ambaye tena anaripoti kwake kinatia mashaka zaidi kama haki itatendeka, Naombeni ushauri wa kitaalamu kuhusiana na hili.