Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
KUMKOSOA SANA NI DALILI KUWA HUYO SIO WAKO BALI UNAMLAZIMISHA AFANANE NA UMTAKAYE.
Karibu kila mtu ana taswira ya nani anamtafuta kama mwenzi/rafiki hivyo siku ukikutana naye utamtambua kuwa ndiye kutokana na kuendana na sifa utakazo.
Kosa kubwa tufanyalo ni kumlazimisha ambaye siye ili awe ndiye na hapo ndipo wengi tunageuka washauri wa mahusiano yetu wenyewe kwa muda mwingi kwa lengo la kutaka awe yule ambaye unamtaka.
Ukiona kwa asilimia kubwa unamkosoa sana ili abadilike jua tayari upo kwa mtu ambaye siye sasa unafanya zoezi la kumbadilisha awe ndiye.
Kitu kigumu kuhusu binadamu kadri unavyoongeza juhudi za kumbadilisha naye anaongeza juhudi za kubaki vile alivyo kwa sababu ki asili binadamu hapendi kubadilishwa.
Kuna kanuni moja nzuri na ngumu hapa isemayo ikiwa huwezi kumpenda alivyo basi mwacha alivyo tofauti na hapo utageuka mshauri na mkosoaji wake kila siku
#Mwanasayansi Saul kalivubha.
#Mitandaoni fikia ndoto zako