Kumlaumu kocha kwa kumtoa Chama ni kuikosea heshima taaluma yake

Kumlaumu kocha kwa kumtoa Chama ni kuikosea heshima taaluma yake

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Kila kocha uwa anao mfumo wake na aina ya wachezaji anaowataka kwenye mfumo husika, kitendo cha kumtoa chama kocha ameona aendani na kile anachokitaka hasa kasi kati kati ya uwanja, uyu kocha inaonekana ni muumini wa soka la kasi ndio maana amewakubali kina kibu denis wakati mashabiki wanawakataa.

Chama kwa soka lake la kutembea kama kinyonga ajiangalie sana anaweza kuwa anaanzia benchi mbele ya uyu kocha vinginevyo ajirekebishe na hiyo ndio hasara ya kubadilisha makocha bila mpangilio, kuna watakaonufaika na kocha mpya na kuna watakaorudi benchi.

Kwa maana hiyo asilaumiwe kocha yeye ndiye anayejua anataka nini kwenye kuijenga timu anayotaka, Mashabiki mnaomuona chama kama Mungu mtu jiandaeni kisaikolojia
 
Kocha anajua kusoma mchezo na kufanya marekebisho haraka. Alifanya marekebisho game na CSK yakaleta matunda.

Hii ilikuwa ni weakness watu wanailalamikia kwa Mgunda. Cha muhimu apunguze experiments au achague game sahihi za kufanya majaribio. Wakati mwingine ni busara zaidi kuplay safe.

Pia Kibu anahitaji msaada wa kisaikolojia, apewe mapumziko hayupo sawa. Hili nimelisema sana humu.
 
Kocha anajua kusoma mchezo na kufanya marekebisho haraka. Alifanya marekebisho game na CSK yakaleta matunda. Hii ilikuwa ni weakness watu wanailalamikia kwa Mgunda. Cha muhimu apunguze experiments au achague game sahihi za kufanya majaribio. Wakati mwingine ni busara zaidi kuplay safe.

Pia Kibu anahitaji msaada wa kisaikolojia, apewe mapumziko hayupo sawa. Hili nimelisema sana humu.
Mechi dhidi ya CSK Moscow, wachezaji wote waliocheza kipindi cha kwanza walitolewa hadi kipa
 
Mechi dhidi ya CSK Moscow, wachezaji wote waliocheza kipindi cha kwanza walitolewa hadi kipa
Sawa, nimepokea marekebisho hayo nilidhani CSK pekee ndiyo walibadili timu nzima maana sikuangalia game yote.
 
Kocha anajua kusoma mchezo na kufanya marekebisho haraka. Alifanya marekebisho game na CSK yakaleta matunda.

Hii ilikuwa ni weakness watu wanailalamikia kwa Mgunda. Cha muhimu apunguze experiments au achague game sahihi za kufanya majaribio. Wakati mwingine ni busara zaidi kuplay safe.

Pia Kibu anahitaji msaada wa kisaikolojia, apewe mapumziko hayupo sawa. Hili nimelisema sana humu.
Kibu ni yule yule[emoji1]
 
Ni either Kocha atafute namna Chama aingie kwenye mfumo wake, au Kocha aingie kwenye mfumo wa Chama. Tunachotaka sisi Chama acheze basi...
 
Back
Top Bottom