Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimemaanisha CSKA MOSCOW walibadili timu nzima kipindi cha pili. waliocheza kipindi cha kwanza hawakucheza tena kipindi cha piliSawa, nimepokea marekebisho hayo nilidhani CSK pekee ndiyo walibadili timu nzima maana sikuangalia game yote.
Hilo mbona na mimi nilisema kwenye post yangu? Nikasema Robertinho alibadili baadhi ya wachezaji wa Simba na ndiyo wakaenda kubadili mchezo kipindi cha pili.Nimemaanisha CSKA MOSCOW walibadili timu nzima kipindi cha pili. waliocheza kipindi cha kwanza hawakucheza tena kipindi cha pili
Nmeshangaa aisee!! Chama yeye kama nani?Mwalimu aingie kwenye mfumo wa Chama au?
Kisinda na mambio yake kuliko chama kuna lipi alilofanya?Kila kocha uwa anao mfumo wake na aina ya wachezaji anaowataka kwenye mfumo husika, kitendo cha kumtoa chama kocha ameona aendani na kile anachokitaka hasa kasi kati kati ya uwanja, uyu kocha inaonekana ni muumini wa soka la kasi ndio maana amewakubali kina kibu denis wakati mashabiki wanawakataa.
Chama kwa soka lake la kutembea kama kinyonga ajiangalie sana anaweza kuwa anaanzia benchi mbele ya uyu kocha vinginevyo ajirekebishe na hiyo ndio hasara ya kubadilisha makocha bila mpangilio, kuna watakaonufaika na kocha mpya na kuna watakaorudi benchi.
Kwa maana hiyo asilaumiwe kocha yeye ndiye anayejua anataka nini kwenye kuijenga timu anayotaka, Mashabiki mnaomuona chama kama Mungu mtu jiandaeni kisaikolojia
Hiyo Simba hatuitaki! Tusipokuwa makini na hisia zetu hatutoboi kokote hata na huyo Mgunda.Kama kocha haingii kwenye mfumo wa chamaaa Hana maisha marefu Simba.
Umeshasema kocha anajua kusoma mchezo, ajabu unamwambia tena apunguze experiments, acheze safe, ukimaanisha awe muoga..Kocha anajua kusoma mchezo na kufanya marekebisho haraka. Alifanya marekebisho game na CSK yakaleta matunda.
Hii ilikuwa ni weakness watu wanailalamikia kwa Mgunda. Cha muhimu apunguze experiments au achague game sahihi za kufanya majaribio. Wakati mwingine ni busara zaidi kuplay safe.
Pia Kibu anahitaji msaada wa kisaikolojia, apewe mapumziko hayupo sawa. Hili nimelisema sana humu.
Kocha ndio abadilike ajue namna ya kumtumia Chama na akishindwa hivyo bora atuachie timu yetu ...... hatuwezi kuwa na kocha anayemfanyia sub Chama dk 34 tu hiyo sio Simba tunayoitaka na hata angeshinda 5 kwa ujinga ule siwezi kukubaliKòcha kaja na mifumo yake, kikubwa ni kwamba hawa makocha wazungu huwa na misimamo na wanaamini ktk taaluma zao na hawakubali kupangiwa.
Chama abadilike acheze kocha anavotaka au chama akae bench
Kweli watu tunatofautiana ufahamu wa haya mambo. Moja ya mapungufu ya Simba tena niliwahi kuyasema sana humu ndani yalikuwa kupenda au kulazimika kurudisha mipira nyuma sana na kushindwa kupenetrate mipira pale kati. Jana hatukuona mapungufu yale. Tuliona hata timu inabadili uwanja kwa mipira mirefu. Wengine wanaita hiyo butua butua lakini hiyo ni timu inayojua kutanua uwanja. Jana kungekuwa na safu nzuri pale mbele, Simba alikuwa na goli kama 3 zaidi.-Mpira siyo riadha, mpira wa sasa ni fani,na weledi
-Jana mpira ulitambaa badala ya kutembea, bado kuna kazi ya kufanya kufikia malengo ya klabu.
-Kama mwendo ndiyo huu,sioni utulivu na amani ndani ya klabu ya SIMBA,na Kocha mpya atafungusha virago vyake mapema.
-Mwekezaji ametumia karibu billion 2 Dubai kwa mpira ule.
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
SikupingiUmeshasema kocha anajua kusoma mchezo, ajabu unamwambia tena apunguze experiments, acheze safe, ukimaanisha awe muoga..
Hakuna kocha anayejitambua hapa duniani atafuata ushauri wako, kuwa kocha ni kuchukua maamuzi magumu bila kujali matokeo ya mwisho, akishinda anasifiwa, timu ikifungwa lawama zinaenda kwake mkitaka mfukuzeni, hayo ndio maisha ya makocha wenye akili zao.
Hatutaki makocha waoga wanaoogopa hata kufanya sub, timu inakuwa static haitembei, mbinu hizo hizo muda wote wa mchezo, bila kujali kama mpinzani wako amebadilisha mbinu zake, matokeo yake ni kufungwa kipindi cha pili tu..