Habari wadau
Kuna familia imepata msiba wa mama yao. Mama huyo amefariki kwa mateso makali ya kuugua kwa zaidi ya miaka 10. Mama huyo alikuwa na cancer na Stroke pia.
Familia imeuza mali zao karibu zote katika harakati za kumtibia mama yao na mateso ya kisaikolojia ya kuuguza wamepitia sana kama familia.
Cha kushangaza baada ya mama yao kufariki Jumuiya na kanisa inawalazimisha wakatoe sadaka ya shukrani Kanisani.
Familia inajiuliza kwa nini tukatoe sadaka hiyo? Maana ni sawa sawa na kwenda kumshukuru Mungu kwa kumtesa mama yao kwa magonjwa makali. Yaani mgonjwa ateseke miaka 10 na bado wakatoe sadaka ya kushukuru mateso hayo? Huyo anayetaka sadaka kwa nini hakuzuia mgonjwa asipate maumivu na mateso ili apate sadaka ya kushukuru kweli kwa kumponya mgonjwa?
Kwa upande wangu naona familia ipo sahihi, kwa upande wenu wadau mnaonaje hili ?