Gwappo Mwakatobe
R I P
- Nov 22, 2019
- 1,796
- 2,345
Kumeibuka na tabia fulani ya kumshindanisha Mheshimiwa Samia na hayati Magufuli kwenye kila jambo na hatua anazochukua.
Mfano, kwenye hafla ya kupokea ripoti ya CAG mheshimiwa aliagiza kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa Bandari, baada ya hatua hiyo kuliibuka na wachambuzi uchwara wakaanza kulinganisha hatua hiyo na hatua ambazo buriani angeweza kuchukua. Mara angekuwa Magufuli angevunja mpaka bodi ya bandari mara sijui angefanyaje, kwa kifupi ni maneno mengi sana yalisemwa siku hiyo.
Kadhalika kumeibuka tabia ya watu kumlazimisha mheshimiwa kuvaa viatu vya hayati jpm kwa maana ya kufanya mambo yale yale aliyoyafanya Magufuli wakati wa uhai wake. Hii ni tabia ya hovyo ambayo si tu inafaa kukemewa bali kupingwa na kila mtu mwenye akili timamu sababu tabia hii inalenga kuingilia majukumu ya kiti cha Urais hivyo kumfanya Mheshimiwa Samia kutekeleza majukumu yake katika wakati mgumu.
Ni kweli, kwamba kuna mengi mazuri yalifanywa na buriani Magufuli na baadaye Mungu ikampendeza akamchukua. Mazuri yake tutayachukua na kuyaenzi lakini kisiwe kigezo cha kumlinganisha na mama Samia kwa sababu Urais sio mashindano bali ni njia tu ya kuwatumikia watanzania kwa lengo la kuwaletea maendeleo.
Kwa hivyo wana CCM wenzangu wakiwemo wabunge, viongozi na watanzania wote kwa ujumla tuache tabia ya kumlinganisha Magufuli na Mh. Samia bali tumwache Rais afanye kazi yake kwa uhuru na sisi kama wanachi tumpe ushirikiano wa kutosha ili atuvushe tutoke hapa tulipo twende mbele zaidi.
Wanafunzi wafuatilie hotuba zake, dah ingekuwa shida sanaMwendazake Kisha enda, huyu jamaa alijua atakufa soon ndio maana akawa analazimisha aingizwe kwenye vitabu vya kiada vya historia
Ni vita kati ya CCM mpya na CCM ya zamani. Mpaka sasa ubao unasomaHuenda ni Conflict kati ya CCM Mpya na ya Zamani! CCM Mpya huenda ina wasiwasi ya ku loose battle kwa CCM ya Zamani.
Kuna ajenda ya siri nyuma ya hayaMimi nashangaa kuna mataga yanamlinganisha Mh Samia na vitu vya ajabuajabu 🥺
HAO NI SUKUMA GANGKumeibuka na tabia fulani ya kumshindanisha Mheshimiwa Samia na hayati Magufuli kwenye kila jambo na hatua anazochukua.
Mfano, kwenye hafla ya kupokea ripoti ya CAG mheshimiwa aliagiza kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa Bandari, baada ya hatua hiyo kuliibuka na wachambuzi uchwara wakaanza kulinganisha hatua hiyo na hatua ambazo buriani angeweza kuchukua. Mara angekuwa Magufuli angevunja mpaka bodi ya bandari mara sijui angefanyaje, kwa kifupi ni maneno mengi sana yalisemwa siku hiyo.
Kadhalika kumeibuka tabia ya watu kumlazimisha mheshimiwa kuvaa viatu vya hayati jpm kwa maana ya kufanya mambo yale yale aliyoyafanya Magufuli wakati wa uhai wake. Hii ni tabia ya hovyo ambayo si tu inafaa kukemewa bali kupingwa na kila mtu mwenye akili timamu sababu tabia hii inalenga kuingilia majukumu ya kiti cha Urais hivyo kumfanya Mheshimiwa Samia kutekeleza majukumu yake katika wakati mgumu.
Ni kweli, kwamba kuna mengi mazuri yalifanywa na buriani Magufuli na baadaye Mungu ikampendeza akamchukua. Mazuri yake tutayachukua na kuyaenzi lakini kisiwe kigezo cha kumlinganisha na mama Samia kwa sababu Urais sio mashindano bali ni njia tu ya kuwatumikia watanzania kwa lengo la kuwaletea maendeleo.
Kwa hivyo wana CCM wenzangu wakiwemo wabunge, viongozi na watanzania wote kwa ujumla tuache tabia ya kumlinganisha Magufuli na Mh. Samia bali tumwache Rais afanye kazi yake kwa uhuru na sisi kama wanachi tumpe ushirikiano wa kutosha ili atuvushe tutoke hapa tulipo twende mbele zaidi.
Tuna wafahamu na mipango yao ya kumhujumu Rais tumeshainyakaHAO NI SUKUMA GANG
Asante kwa appreciation mkuuUshauri mwanana