Kumng'oa Mangungu Simba ni vigumu kama kuing'oa CCM madarakani

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Huyu mtu yupo pale kutumika kisiasa. Amewekwa na wanasiasa na kwa nguvu zao sioni iwapo ataacha madaraka yake.

Nikisikiliza jinsi anavyojibu kijeuri, sipati shaka kabisa kuwa Simba kwa sasa inaanguka anguko kubwa sana. Huenda kuna siri hatuijui lakini wanasimba tuanze kujifunza kuishi kama mashabiki wa Ihefu.

Hakuna matumaini kwa sasa hawa jamaa wakiwapo madarakani. Wanachama wenyewe wapiga kura wa Simba ndio hao wanaume wa Dar. Asilimia kubwa machawa na hawajitambui. Mimi sina matumaini kuwa Simba itatulia tukiwa na hawa viongozi.

Engineer amesema atatunyoosha! Na tutanyooshwa sana. Maana hata mwekezaji ni tatizo jingine.
 
Mangungu hahusiki kwenye daily operation za Simba, ni kiongozi asiye na nguvu kutokana na katiba mpya ya Simba. Try again na CEO wake na MO ndio wenye mamlaka na maamuzi, inahitajika kuwe na uwazi kuelewa tatizo la usajili la Simba, je ni pesa ndogo au ni uzembe wa scouting team ? Simba ina chief scout yule mzungu wa Uholanzi anafaa kuwa katika top list ya wanaofukuzwa.
 
Tatizo kubwa la Simba ni wanachama wake tofauti na yanga ambao wanachama wao linapokuja swala la timu wanaweka maslahi ya timu mbele Ila Simba wanachama wapo tayari kuongea ili mradi wapate chochote badala ya kuangalia maslahi ya timu.
Mo Dewji kwa kutambua Aina ya wanachama walioko Simba ndio maana anaweka viongozi anaowataka na pia amehakikisha wanachama wapya hawaingizwi badala yake amekuwa akiingiza wanachama wanasiasa Kama wabunge.
Ada ya uwanachama kwa mwaka hazizidi 120000 lakini mapato ya mchango wa wanachama hauzidi 30000000 ukigawanya ni Kama wanachama 250 wanachangia.
Kama Simba ikianza kusajili wanachama ni wazi wataingiza pesa nyingi ndipo watashituka na kujua pesa aliyotoa mo ni ndogo Sana.
 
Ushauri wa bure kabisa kwa huyo Mangungu na hata Try Again wajiuzulu tu Simba kwa sasa ili kulinda heshima yao kidogo iliyobaki wawachie wengine waendelee wao walipoishia. Na wakati sahihi ni sasa hivi wasisubiri mpaka msimu mpya uanze. Kwa ninavyozijua hizi timu za Kariakoo ikifika mahali mashabiki, wapenzi na wanachama wamechoka kwa kweli hao viongozi watakuja kuondoka kwa aibu kubwa sana.
 
Mangungu alipaswa kujiuzulu na kuweka wazi udhaifu wowote ili ufanyiwe kazi.
Kwa sasa anauluzwa tatizo nini,yeye anasema wanasubiri taarifa kutoka sehemu mbali mbali ili wafanye tathmini.
Wenzao wanafanya tathmini wakati mechi zinaendelea na kuanza usajili mapema,wao wakae kwanza,waanze majungu,ndipo dakika za mwisho wakatuletee akina sawadogo na jobe wengine.Halafu wanawekeza nguvu kwenye propaganda.Huu ni uzembe na uhuni wa hali ya juu
 
Toa sababu kumi kwanini ni ngumu kung'oola hapo msimbazišŸ¤”
 
Orodha aliyowasilisha scout wa Simba kwa wachezaji kusajiliwa hakuna hata mmoja aliyesajiliwa mojawapo ni Pacome Zouzoua na Mohamed Zougrana.

Simba waienda kumsajili Zouzoua lakini Try again akaamua kumsajili Aubin Kramo
 
Simba imezuiliwa kusajili wanachama wapya mpaka mchakato wa mabadiliko ukamilike acheni kuokoteza taarifa
 
Kabla ya No Simba walikuwa wakisajili wanachama hiyo hela kubwa ilikuwepo ?
 
Simba ni Shwari hamna Shari...!

Majirani mnataka ionekane kuna Timbwili...!
Hafukuzwi mtu, Hang'oki mtu....!
Simba Nguvu 1....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…