Ndugu zangu Wazaramo huwa na neno moja wanaliita Bangusilo, yaani pangusio. Naona hapa Mangungu kaanza kutumika kama Bangusilo.
Kwamba Mangungu ndiye kafanya timu isimalize ligi ikiwa kwenye nafasi mbili za juu. Ndiye kachaguliwa atajwe kuwa chanzo cha kukosa ubingwa.
Yaani mjumbe wa bodi kama alivyo Asha Baraka ndiye awe na nguvu utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya timu kuliko CEO na Mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi.
Wanasimba, kikatiba Mangungu hana nguvu yoyote kwenye timu, zaidi ya kuwawakilisha wanachama kwenye kikao cha Bodi ya Simba.
Kama tuna hamu sana ya kumpa Mangungu lawama tukikosa ubingwa, basi kwanza tubadilishe katiba yetu na tumpe hiyo nguvu.
Tulifanya makosa kupitisha katiba ile inayompa nguvu hafifu mwakilishi wa wanchama (Mangungu) kwenye vikao vya maamuzi.
Ikumbukwe kuwa, wanachama ndiyo wenye hisa nyingi kuliko mwekezaji, ila katiba inampa mwekezaji nguvu ya maamuzi, ni upuuzi.
Ova