Kumnyima upadre anayestahili kunaleta maumivu makubwa sana. Ya Prof Maghway ni ushuhuda

Kumnyima upadre anayestahili kunaleta maumivu makubwa sana. Ya Prof Maghway ni ushuhuda

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
2,828
Reaction score
3,579
PROFESA mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Josephat Maghway (65) jana aliamua kufunga nadhiri za daima za maisha ya utawa katika Kanisa Katoliki la Salvatorian la Chuo Kikuu cha Jordan mkoani Morogoro.

Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata jana kupitia marafiki wa karibu wa Profesa huyo, zilieleza kuwa, kabla ya kuingia utawa na kufunga nadhiri hizo, aligawa vitu vyote ikiwamo nyumba, magari na mashamba kwa taasisi za dini.

“Leo (jana) ndio amefunga nadhiri za daima za maisha ya utawa ambapo amekula kiapo cha kuishi maisha ya kujitolea kwa ajili ya watu maskini kwa kuuza kila alicho nacho na kuwagawia maskini na yeye kuamua kuishi maisha ya nadhiri ya ufukara, utii, na usafi wa moyo,” alisema Faraja Chrysostom ambaye ni rafiki wa karibu.

Alisema ingawa Profesa Maghway anapenda kuishi kitawa lakini shirika lake likitaka linaweza kumpatia upadri.

Akielezea tukio hilo la kuweka nadhiri, alisema Profesa huyo aliungana na watawa wengine wanne wa shirika la Mtakatifu Francis wa Assizi wa Kapuchini walioko Kola, Morogoro kufanya agano hilo.

Profesa Maghway alistaafu kufanya kazi UDSM akiwa na miaka 60 mwaka 2010 na inaelezwa hakuwahi kuoa wala hana watoto.

Profesa Maghway alipongezwa na watu mbalimbali wakiwamo marafiki zake ambao waliandika katika mtandao wa Whatsapp.

Miongoni mwa waliompongeza ni Dk. Vincensia Shule wa kitengo cha Sanaa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye aliandika katika kundi moja la mtandao wa Whatsapp kuwa;

“Kwa namna ya kipekee kabisa napenda kumpongeza Prof. Josephat Baran Maghway kwa kuweka nadhiri ya kudumu ya Utawa…amefanya mengi kwenye taaluma akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Department of Foreign Languages & Linguistics (kitengo cha lugha) sasa ameamua kuendelea kumtumikia Mungu kwa next level (hatua nyingine mbele), Inshallah atakamilisha safari ya upadre”.

HABARI NI YA MWAKA 2017 LAKINI NIMEIONA LEO MTANDAONI.
NIMEIWEKA HAPA KWA SABABU NAMFAHAMU PROF MAGHWAY BINAFSI, ALIKUWA MWALIMU WANGU MLIMANI.
ALINYIMWA UPADRI AKIWA KIJANA, BAADA YA KUSOMA SEMINARINI HADI HATUA YA USHEMASI AKIMALIZA PHILOSOPHY NA THEOLOGY KAMA IPASAVYO. LAKINI KWAKUWA HUO HASA NDIO ULIKUWA WITO WAKE, ALIUISHI HADI UZEENI JAPO ALINYIMWA UPADRE!
MUNGU AZIDI KUMTIA NGUVU.

MAASKOFU NA WENGINE MNAOHUSIKA MUWE MAKINI SANA NA OMBENI UONGOZI WA MUNGU KATIKA TAFAKARI ZENU MNAPOLETEWA MAPINGAMIZI YA KUNYIMA SHEMASI UPADRI, MUNGU AWAONGOZE KATIKA KUTAMBUA WENYE WITO HALISI NA KUWALINDA NA KUWAJENGA.
 
KUPANGA NI KUCHAGUA, ANAKARIBISHWA SANA KWENYE WITO WETU HUU
 
Daaaaah umenikumbusha mbali....I am forever grateful for him from the bottom of my heart.
Tulikua tunasema prof.Maghway ni walking dictionary kwenye phonology hata umuulize swali gani kwa mtego ali transcribe he will do so bila kukosea!!!
Mara nyingi alikua analala ofisini kwake nyuma ya desk lake kuna godoro asbh ukipata unakuta ana nawa yuko na paka wake. He was an interesting person with a unique lifestyle.
Ukienda ofisini kwake if you have an issue haruhusu uingie u state your problem at the door [emoji1][emoji1]
Nilivyomaliza Uni kuna siku nilimuona mitaa ya posta wearing robes za u padre nadhani alishachukua nadhiri then.
I'm lucky to have been his student!!!

Faraja pia was a good tutor friendly and easygoing!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nice piece ! Mimi pia alikuwa mwalimu wangu UD. Nakumbuka sana kule language laboratory kila mwanafunzi akiwa kwenye booth na yeye akiwa anapatch patch kwenye mic....eh...who's at booth number eleven ?... Mungu ambariki sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kupewa kwenye hatua za mwisho huwa wanatangaza kama ndoa , mwenye pingamizi anapeleka na huwa kipindi cha uchunguzi balaa, shemeji yangu hakupewa kisa Baba yake aliacha mke ambaye ni mama yake akawa anaishi na mademu demu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Profesa Maghway alistaafu kufanya kazi UDSM akiwa na miaka 60 mwaka 2010 na inaelezwa hakuwahi kuoa wala hana watoto.

Je, ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa?

ALINYIMWA UPADRI AKIWA KIJANA, BAADA YA KUSOMA SEMINARINI HADI HATUA YA USHEMASI AKIMALIZA PHILOSOPHY NA THEOLOGY KAMA IPASAVYO. LAKINI KWAKUWA HUO HASA NDIO ULIKUWA WITO WAKE, ALIUISHI HADI UZEENI JAPO ALINYIMWA UPADRE!
MUNGU AZIDI KUMTIA NGUVU.

Je, sababu ni zipi hasa?

MAASKOFU NA WENGINE MNAOHUSIKA MUWE MAKINI SANA NA OMBENI UONGOZI WA MUNGU KATIKA TAFAKARI ZENU MNAPOLETEWA MAPINGAMIZI YA KUNYIMA SHEMASI UPADRI, MUNGU AWAONGOZE KATIKA KUTAMBUA WENYE WITO HALISI NA KUWALINDA NA KUWAJENGA.

Hii inaonesha hakuna Umungu kwenye kazi hizo za kichungaji.
 
Kabla ya kupewa kwenye hatua za mwisho huwa wanatangaza kama ndoa , mwenye pingamizi anapeleka na huwa kipindi cha uchunguzi balaa, shemeji yangu hakupewa kisa Baba yake aliacha mke ambaye ni mama yake akawa anaishi na mademu demu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah! Makosa ya dingi nahukumiwa mtoto!!! Si sawa kabisa
 
Je, ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa?

Je, sababu ni zipi hasa?

Hii inaonesha hakuna Umungu kwenye kazi hizo za kichungaji.
  1. Uwezo wa tendo la ndoa angepimwaje wakati hajawahi kuoa? Kumbuka tendo la ndoa ni halali ndani ya ndoa tu. Hivyo kama Profesa hakulifanya tendo hilo ametimiza kuishika vema amri ya Mungu inayokataza zinaa
  2. Sababu za kukataliwa upadre wanazijua waliomkatalia miaka hiyo ya zamani za ujana wake, lakini kwa dhihirisho la maisha aliyoishi Profesa tangu wakati huo hadi uzeeni ni wazi sababu zile ziliwakosesha waumini padre mzuri sana
  3. Umungu upo, kumbuka siku zote binadamu wameshindanisha akili zao na maelekezo ya Mungu, kama wewe unavyobisha hapa
 
Uwezo wa tendo la ndoa angepimwaje wakati hajawahi kuoa? Kumbuka tendo la ndoa ni halali ndani ya ndoa tu. Hivyo kama Profesa hakulifanya tendo hilo ametimiza kuishika vema amri ya Mungu inayokataza zinaa

Kwa kutumia neno 'tendo la ndoa' nilimaanisha kufanya ngono au kujamiiana.
 
Back
Top Bottom