Mnazareth
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 3,474
- 7,404
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mungu atamsaidia huyo mtu kuepuka vichawishi na vikwazo katika njia iliyowekwa na binadamu.Mungu aliwakabidhi binadamu jukumu la kuchagua binadamu wa kufanya kazi ya Mungu. Changamoto inakuja pale wale binadamu waliopewa jukumu hilo wanapotumia ubinadamu wao kuwapata watumishi wa Mungu.
Yaani ilikuwa hivyo, aliukosa jamani, watu wakamshauri yule Mzee aligoma kabisa, zamani kijana anayezaliwa nje ya ndoa ilikuwa ngumu sana kwenda seminary, lazima atoke familia yenye maadili kabisaDaaah! Makosa ya dingi nahukumiwa mtoto!!! Si sawa kabisa
RC wanajua siri nyingi uongozi wao upo mpaka chini kabisa hivyo waumini wanawafahamu vizuri sana, hata wewe unaweza kuwa na jirani yako usimfahàmu mambo yake lakini Padri wako/ wake anayafahamusi kweli, wanaoamua ni wanadamu na mara nyingine wanakosea sana
Hata kaka angu alitoswa Kasita seminary kisa wazaz hawakuwa wamefunga ndoa wakati huo.Yaani ilikuwa hivyo, aliukosa jamani, watu wakamshauri yule Mzee aligoma kabisa, zamani kijana anayezaliwa nje ya ndoa ilikuwa ngumu sana kwenda seminary, lazima atoke familia yenye maadili kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanajua siri zipi? Mbona kuna mtu alikuwa anafahamika na wenzie huko seminarini kuwa ni shoga lakini kapewa upadri? Waseminari wenzie walimjua lakini hakuna aliyethubutu kumsema kwa sababu pale utakapotakiwa kutoa ushahidi inaweza kuwa mwisho wako, ukafukuzwa wewe akabaki huyo unayemtuhumu. Au hata akifukuzwa, inabakia historia pale kuwa wewe ndiwe uliyemfukuzisha, wenzio wanakuchukia na kukuundia zengwe la kufa mtu, hautaishi kwa amani. Matokeo yake waseminari wenyewe ni mabingwa wa kufichiana dhambi.RC wanajua siri nyingi uongozi wao upo mpaka chini kabisa hivyo waumini wanawafahamu vizuri sana, hata wewe unaweza kuwa na jirani yako usimfahàmu mambo yake lakini Padri wako/ wake anayafahamu
Sent using Jamii Forums mobile app
Alifikia levo ipi ?unaposema kukaribia ndio kupi huko?Hata IGP wa sasa Simon Sirro aliachishwa upadri akiwa anakaribia sana kuupata, na kama mnavyomwona ni mtu timamu sana na mweledi, na ana familia. Hizo hadithi nyingine wanazolishana watu ni uzushi tu.
Acha uongo karugendo hakusoma segerea kasoma kipalapala tabora.. stori ya kuungaWanajua siri zipi? Mbona kuna mtu alikuwa anafahamika na wenzie huko seminarini kuwa ni shoga lakini kapewa upadri? Waseminari wenzie walimjua lakini hakuna aliyethubutu kumsema kwa sababu pale utakapotakiwa kutoa ushahidi inaweza kuwa mwisho wako, ukafukuzwa wewe akabaki huyo unayemtuhumu. Au hata akifukuzwa, inabakia historia pale kuwa wewe ndiwe uliyemfukuzisha, wenzio wanakuchukia na kukuundia zengwe la kufa mtu, hautaishi kwa amani. Matokeo yake waseminari wenyewe ni mabingwa wa kufichiana dhambi.
Chanzo cha bifu kati ya padre Privatus Karugendo (ameshaachishwa) na aliyekuwa askofu wake Severini Niwemugizi ni dhambi walizokuwa wanafichiana walipokuwa seminari Segerea, na huyu Karugendo alipoasi akaamua kuzimwaga hadharani. Kwa hekima yake, askofu aliamua kutokumjibu, kwahiyo kashfa akabaki nazo Karugendo hadi leo.
Kwa ujumla jambo likishategemea akili za binadamu pekee haliwezi kuwa na ukamilifu mbele za Mungu.
shemasiAlifikia levo ipi ?unaposema kukaribia ndio kupi huko?
kwahiyo hakusoma na Niwemugizi?Acha uongo karugendo hakusoma segerea kasoma kipalapala tabora.. stori ya kuunga
Kwa siku hizi sidhani kama ipo applicable tena kuna masharti yamelegezwa.Daaah! Makosa ya dingi nahukumiwa mtoto!!! Si sawa kabisa
Hongera kwake.PROFESA mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Josephat Maghway (65) jana aliamua kufunga nadhiri za daima za maisha ya utawa katika Kanisa Katoliki la Salvatorian la Chuo Kikuu cha Jordan mkoani Morogoro.
Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata jana kupitia marafiki wa karibu wa Profesa huyo, zilieleza kuwa, kabla ya kuingia utawa na kufunga nadhiri hizo, aligawa vitu vyote ikiwamo nyumba, magari na mashamba kwa taasisi za dini.
“Leo (jana) ndio amefunga nadhiri za daima za maisha ya utawa ambapo amekula kiapo cha kuishi maisha ya kujitolea kwa ajili ya watu maskini kwa kuuza kila alicho nacho na kuwagawia maskini na yeye kuamua kuishi maisha ya nadhiri ya ufukara, utii, na usafi wa moyo,” alisema Faraja Chrysostom ambaye ni rafiki wa karibu.
Alisema ingawa Profesa Maghway anapenda kuishi kitawa lakini shirika lake likitaka linaweza kumpatia upadri.
Akielezea tukio hilo la kuweka nadhiri, alisema Profesa huyo aliungana na watawa wengine wanne wa shirika la Mtakatifu Francis wa Assizi wa Kapuchini walioko Kola, Morogoro kufanya agano hilo.
Profesa Maghway alistaafu kufanya kazi UDSM akiwa na miaka 60 mwaka 2010 na inaelezwa hakuwahi kuoa wala hana watoto.
Profesa Maghway alipongezwa na watu mbalimbali wakiwamo marafiki zake ambao waliandika katika mtandao wa Whatsapp.
Miongoni mwa waliompongeza ni Dk. Vincensia Shule wa kitengo cha Sanaa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye aliandika katika kundi moja la mtandao wa Whatsapp kuwa;
“Kwa namna ya kipekee kabisa napenda kumpongeza Prof. Josephat Baran Maghway kwa kuweka nadhiri ya kudumu ya Utawa…amefanya mengi kwenye taaluma akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Department of Foreign Languages & Linguistics (kitengo cha lugha) sasa ameamua kuendelea kumtumikia Mungu kwa next level (hatua nyingine mbele), Inshallah atakamilisha safari ya upadre”.
HABARI NI YA MWAKA 2017 LAKINI NIMEIONA LEO MTANDAONI.
NIMEIWEKA HAPA KWA SABABU NAMFAHAMU PROF MAGHWAY BINAFSI, ALIKUWA MWALIMU WANGU MLIMANI.
ALINYIMWA UPADRI AKIWA KIJANA, BAADA YA KUSOMA SEMINARINI HADI HATUA YA USHEMASI AKIMALIZA PHILOSOPHY NA THEOLOGY KAMA IPASAVYO. LAKINI KWAKUWA HUO HASA NDIO ULIKUWA WITO WAKE, ALIUISHI HADI UZEENI JAPO ALINYIMWA UPADRE!
MUNGU AZIDI KUMTIA NGUVU.
MAASKOFU NA WENGINE MNAOHUSIKA MUWE MAKINI SANA NA OMBENI UONGOZI WA MUNGU KATIKA TAFAKARI ZENU MNAPOLETEWA MAPINGAMIZI YA KUNYIMA SHEMASI UPADRI, MUNGU AWAONGOZE KATIKA KUTAMBUA WENYE WITO HALISI NA KUWALINDA NA KUWAJENGA.
Ni kweli !! Sio sawa kabisaDaaah! Makosa ya dingi nahukumiwa mtoto!!! Si sawa kabisa