Kumpenda nampenda ila mimi ni aina ya mtu nisiyependa kuongea kwa simu

Kumpenda nampenda ila mimi ni aina ya mtu nisiyependa kuongea kwa simu

Mwanaume ukishafikia stage ya kusema Kumuacha Hapana basi kwisha habari yako.Narudia hakuna Mapenz over the phone,ni swala la muda tu [emoji1]
Otherwise ni mke mpo naye mbali kikazi..ila vinginevyo kwanza ni ghali mnoo kudate na mtu akiwa mbali,,kuanzia nauli n.k
 
Tuko mbali mikoa tofauti, hapa kisanga ndipo kinakuja. Anapenda kupiga piga simu mara kwa mara, sasa mara nyingi najikuta namkatiza ilee.. "Samahani ngoja nitakupigia baadae kidogo".

Kiukweli muda huo unakuta shughuli imenitinga na ukizingatia aina ya shughuli zangu haziruhusu sana kuongea kwa simu muda mrefu la si hivyo zitayumba. Sasa na anakupigia unakuta cha maana cha kuongea hana, ukimdodosa ni kwamba labda anapenda tu kusikia sauti yako.😂

Ukirudi usiku umechoka unataka uoge upumzike, ukipiga simu ni muongee zaidi ya dakika 40+, wengine mnawezaje? Nahofia kuja kumkwaza.

Hili swala hata ndugu zangu walishanizoea, mimi huwa nikipiga simu nina jambo la msingi la kuzungumza. Napendelea zaidi text kuliko kupiga simu. OMG sijui ni huu usukuma wangu. Sasa na haya mahusiano ya mbalimbali tutafika kweli?🚶🏿
🤔🤔Fimbo yambali hauwi nyoka! Sijui wahenga waliwaza nn😶
 
Long distance relationship tushasema ni entertainment hizo,hakuna kitu kinaitwa long distance r.ship,achana nae fanya mambo yako tu

Kama hajakuelewa na hapa basi soon tutazika huyu jamaa [emoji28]
 
Tuko mbali mikoa tofauti, hapa kisanga ndipo kinakuja. Anapenda kupiga piga simu mara kwa mara, sasa mara nyingi najikuta namkatiza ilee.. "Samahani ngoja nitakupigia baadae kidogo".

Kiukweli muda huo unakuta shughuli imenitinga na ukizingatia aina ya shughuli zangu haziruhusu sana kuongea kwa simu muda mrefu la si hivyo zitayumba. Sasa na anakupigia unakuta cha maana cha kuongea hana, ukimdodosa ni kwamba labda anapenda tu kusikia sauti yako.😂

Ukirudi usiku umechoka unataka uoge upumzike, ukipiga simu ni muongee zaidi ya dakika 40+, wengine mnawezaje? Nahofia kuja kumkwaza.

Hili swala hata ndugu zangu walishanizoea, mimi huwa nikipiga simu nina jambo la msingi la kuzungumza. Napendelea zaidi text kuliko kupiga simu. OMG sijui ni huu usukuma wangu. Sasa na haya mahusiano ya mbalimbali tutafika kweli?🚶🏿
Maongezi yangu marefu kuwahi kuongea ilikuwa 60-70 minutes......
Yalobakia ni mafupi kama shoo ya kuku
 
Mtafika tu..kikubwa mwanamke anatakiwa aelewe situation yako au wewe ubadilike kwa ajili yake.
 
Hana story au story zake zinakuboa.
Yaani hebu nijaribu mimi uone kama hatutakuwa tunaongea na simu hadi voda wanaamua kukata wenyewe
zinakuwepo but na uchovu unakuta unachangia ticha si unajua huu mji na pirika zake.
 
Yani kazi tunayo mkuu,kesi kila siku haziishi ,ukiwaambia hakuna mapenz kweny long distance wnakua wakali,yakiwakuta wanakuja kulia nyau humu,sasa mimi nimemwambia achana nae uyo,kasema HAPANA [emoji1][emoji23]
....anajifanya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterez, acha yamkute.
 
Mkuu, tuko wote! Siwezi kabisa zungumza na simu kwa muda wa zaidi ya sekunde 30, sijui kumbebisha mtu kwa simu aisee!
 
Badilika just for her... Halafu kwa LDR mawasiliano ni muhimu na msingi sana otherwise............!
 
Badilika just for her... Halafu kwa LDR mawasiliano ni muhimu na msingi sana otherwise............!
Ndo kilichonikuta LDR jau unamuona mtu anajisnap tu boda wake alafu anakwambia umsaidie kitu flani nikamuulize yule unaejisnap nae hana mnasaada?

Ndo ugomvi ukaanza na mahusiano kufa
 
Ndo kilichonikuta LDR jau unamuona mtu anajisnap tu boda wake alafu anakwambia umsaidie kitu flani nikamuulize yule unaejisnap nae hana mnasaada?

Ndo ugomvi ukaanza na mahusiano kufa
Pole sana mkuu LDR ni changamoto sana!
 
Usikate tamaa. Kama unampenda basi mueleze hilo jambo la kutoweza kupokea simu wakati wa kazi atakuelewa tu.

pili muambie kwamba kama anakuwa bored atafute kitu cha kuchangamsha akili badala ya kuwa kwenye simu masaa ishirini na nne.

Mutafika tu muwe wavumilivu na murekebishane kwa upendo pale mnapoona mmoja wenu amekosea kufanya jambo fulani katika mahusiano yenu.

Ninakuambia hivyi kwa sababu nilidhawahi kuwa kwenye LDR mwaka jana haikuwa rahisi sana ila nilijifunza mengi sana. sema mahusiano yetu yalikuwa kwa muda wa miezi minne tu tuliachana kwa sababu za kijinga tu.
I hope alipata mwenza mzuri wa maisha.

So follow your heart.
 
Back
Top Bottom