Nimeona Watanzania wakichangamka kumpigia kura mchezaji wa Simba SC kwenye moja ya tuzo katika kipengele cha Goli bora la mwaka.
Kiukweli hilo jambo la kuacha watu wapigie kura mshindi limewekwa kimkakati na kibiashara tu.
Uhalisia ni kwamba hawawezi acha majority wasio kuwa na ufahamu wa mpira wapige kura maana CAF wana fahamu kabisa kuna “mambumbumbu” pia yana shabikia mpira hivyo si rahisi kupata mshindi mwenye kustahili.
Aidha, Caf wanafahamu kuwa baadhi ya wachezaji wanatoka kwenye mataifa yenye uwiano mdogo wa population hivyo wale wenye kutoka kwenye mataifa yenye population kubwa watanufaika zaidi hata kama hawastahili.
Ndio maana hata TFF imechagua kamati maalumu kubaini washindi katika tuzo za TFF zilizo tamatika.
Ifuatayo ni orodha ya wapiga kura katika kila kipengere ambacho kitaamua mshindi:-
1. Kamati ya Ufindi ya CAF
2. Waandishi wa Habari/michezo watambulikao CAF
3. Makocha wakuu wa timu shiriki msimu 2021/22
4. Makaptein wa timu shiriki msimu 2021/22
5. Klabu zilizo shiriki makundi msimu 2021/22
Endapo kura zitagongana/kufanana ndipo kura za mashabiki zitatumika.
Ikumbukwe: Tangu CAF ianzishwe mwaka 1957. Hakuna msimu wa tuzo kukatokea kufanana kwa idadi ya kura.