Kumpoteza mtu unayempenda!!

pole sana,haya mambo yametukuta wengi.hasa kama huyo mtu ulimuamini na kumpenda kwa asilimia zote.ila kwa sasa utajisikia unaumwa ugonjwa unaoumwa haujulikani,unajikuta una hasira zisizokuwa na sababu,na mawazo mpaka unajihisi kama kuchanganyikiwa,na maswali yasiyokuwa na majibu.trust me itachukuwa muda,ila baadae utakaa sawa tu,na ipo siku utapata mtu atakaekupenda wewe,na baada vya miaka kadhaa utajiuliza hivi yule mtu alieniumiza kipindi kile upande mwengine niliepuka mengi.maana nina furaha kwa huyu nilie nae.
 
Pole BJ
Usione Mungu amekuacha kwa hili yupo pamoja nawe
huyo hakustaili endelea kumtumaini Mungu atakupa anayestahili
jipe moyo ni mapito ya dunia
.
 

Fuata ushauri wa mmoja wa wanajamvi ambao ndio kinga yangu ninayoitumia ktk love life/relationships. Huu ushauri umenisaidia sana na ninapeta tu sasa hivi kwani when it comes to love...I have a bullet proof heart. Namnukuu:
"mapenzi sio ya kuyaendekeza sana yatakugeuza chizi...just relax and enjoy life,when u met a snitch just quit early

'MIMI NINA MSEMO WANGU AMBAO SIKUZOTE UNATEMBEA KICHWANI...KWAMBA SIKUZALIWA NA MTU NA WALA HAKUNA ALIYEUMBWA KWA AJILI YANGU"


Nina imani huo ujumbe hapo juu utakusaidia.
 
Kabla hujatendwa huo ujumbe hauna maana, ila ikitokea umetendwa una maana saaana.
 

Oh!!! Masikini pole sana mpenzi, yaaani naweza kufikiri inavyokuwa ngumu sana kwa mtu uliyempenda akikutenda. Naomba uupe moyo wako nafasi ya wazi kabisa kwake, ninamaanisha nini: Jitahidi kuifanya akili yako ifikirie yale mambo mabaya aliyokuwa akikufanyia, epuka kabisa kufikiria vitu vizuri alivyokuwa akikutendea/alivyonavyo. Husiutese bure moyo wako kwa kumfikiria, maana yeye hana hata wazo, sana sana atakuwa akifurahia maisha yake mapya na mke wake. Jitahidi sana kufanya kazi kama ni mwajiriwa, kama ni mjasilia mali jitahidi na biashara zako, kama una malengo ya kununua kiwanja, nyumba, gari, au kitu chchote unachoona kinakufurahisha peleka mawazo yako huko, japo naona kama yeye ndo ilikuwa furaha yako, lakini mwenzio ndio hivyo tena. Kama una marafiki/ndugu ambao uanweza ukabadilishana nao mawazo live bila kukukwaza jitahidi kujichanganya nao. Jinunulie vitu vizuri unavyovipenda, viatu, nguo, mashuka, mapazia, badilisha muonekano wa nyumba/chumba. Jitahidi kujipenda zaidi kuliko ulivyokuwa nae. Kidogo kidogo utamsahau, usithubutu kumpigia simu na kumuuliza kwa nini umenifanyia hivyo, kwa sababu haitabadilisha kile alichokifanya sana sana atakudanganya. Kwa kifupi kaa naye mbali kwa kila kitu. Pole sana mpenzi.
 

Samahani ndugu yangu, hapa kidogo mi naona itamtia machungu zaidi huyu ndugu yetu. Kumtafuta na kuonana naye tena hapana big NO!! Maana huwezi juwa huyu jamaa ilikuwaje mpaka akaamua kuoa. Vipi akija na mke wake amtambulishe BJ kuwa huyu ni mke wangu, umeniita nimeona nije naye kabisa umjue, vipi akija amepania kwa kujiweka mtanashati kuanzia mavazi mpaka marashi amtege BJ wa watu, kumbuka BJ anasema anampenda sana, itakuwaje wakinywa wine halafu baadaye wajikute wako ulimwengu wao wa zamani? HAPANA. BJ jitahidi kuishi maisha yako mwenyewe bila kumuuliza alipo, yuko na nani? na anafanya nini? Umesikia mtoto mzuri, kuwa na msimamo wako, wanaume wanapenda wanawake wenye msimamo, husimfuate fuate maadam hakukuthamini na kuoa mwanamke mwingine. JITAHIDI UKAE NAE MBALI, BASI,
 
Kwa faida ya wengi walio/wanao/watakao/pitia hali kama hii, tungeomba mtumie lugha ya kiswahili...tunathamini michango yenu...Tafadhali..mtutafsirie na sisi wengine,

Tunaomba ututafsirie signature yako hapa chini. JUST KIDDING LOL!!!!
 
pole sana mpendwa,
wanaume wanachukizwa na vitu fulani fulani vinvyopelekea kuachana na wapenzi wao..mtafute hata kupitia mtu mwingine akueleze sababu ya KUKUACHA,
Ninauhakika ipo sababu huwezi achwa bila SABABU,tafadhali mtafute atakueleza pengine hapo mwanzo HUKUMSIKILIZA ndio maana KAKUACHA.
JIONO NJEMA
 
Pole sana BJ,

Hebu ichukulie hii hali kama mtu aliyepata msiba. Jipe muda wa kuomboleza na baada ya hapo naamini utasonga mbele bila kuhisi maumivu tena na mateso ingawa pengo litabaki. Kwa kufanya hivyo utaweza kuyakabili maisha kwa imani kwamba huyo mtu hutamwona tena (sina maana akiwa hali bali akiwa wako)!!!!!!
 
sidhani kama alikua mchumba wako,na labda ni mtu tu ulikua una mpenda!
Kama alikua mchumba wako,ulikua wapi toka yuko kwenye "uchumba" mwingine hadi anaoa?

Pole sana,ingia kwenye love connect tuta jitokeza wa kukusahaulisha
 

OMG BJ...! Pole.
You can forgive BUT, you cannot forget (the way he made you feel!)
Hivyo suala la ufanye nini upate kumsahau kwanza ondoa...

Nipo page One, ...naendelea kusoma wachangiaji wengine...
 
Pole sana BJ hivi vitu vipo na na huwa vinapita kwa msaada wa mungu atakuwezesha na utampata wa kwako ambaye atakupenda utampenda na atakayekuthamini,my dear umenikumbusha mbali saaana miaka saba iliyopita ,
Mungu akupe ujasiri wa kukabiliana na hili
 

...suluhisho lako limo hapo kwenye red.
All in all, Life has to go on!

Yeye ameoa, anaendelea na furaha na maisha yake.
Truth Hurts, lakini ni aheri kujua na kuukubali ukweli
kuliko kujua ukweli lakini uendelee kuukana.

The grudge, anger and pain you hold haiku affect wewe pekee,
inaathiri hata marafiki ambao wangependa kukufariji kipindi hiki cha mpito.

Maisha ni mafupi, Let it go!
 
Pole sana BJ na Mungu akupe nguvu za kuweza kuvuka wakati huu mguu na akuletee mwingine ambaye mtapendana zaidi ya huyu.

Kitendo cha huyu mtu kuoa ni sababu kubwa moja ambayo ilitakiwa kukusidia kuhamini kwamba ushampoteza na mda umefika sasa wa ku-move on hata kama ni vigumu vipi. Simama mbele ya kioo na uambie moyo wako kwamba sasa tunasonga mbele huyu mtu hayupo tena. Wewe tu mwenyewe ndio unaweza kujiponya na kujiendeleza hili uweze kujiandaa na yalio mbeleni.

Kwa sasa nakushauri sahau kwamba huyu jamaa peke yake ndio mwenye uwezo wa kutimiza matatizo yako yote ya mapenzi na mengine. Yeye binadamu kama wewe na ana matatizo yake na mapungufu pia.

Na pia jaribu kutambua mapungufu yako yoyote ambayo unahisi yalimfanya aondoke hili uweze kujirekebisha uko mbeleni , kwani binadamu wote sie tuna upande wa pili ambao unaweza kuwa kero kwa wenzetu pia.

Pole sana BJ.
 
Pole sana mpendwa!Alichofanya huyo kaka sio vizuri kabisa..yani binafsi hamna kitu nachukia kama mtu kukutenda kwa namna yoyote ila alafu usipate maelezo.Hua inasumbua sana maana hata ukijaribu kumsahau kuna wakati utajikuta unaanza kujiuliza kwanini and before you know it unaanza kuomboleza upya.Mwenyewe naugulia kwa mbali ila nakuonea wewe huruma zaidi maana mpaka jamaa anatangaza ndoa na kuapa madhabahuni hakua anajali hisia zako hata kidogo.

Nwy unfinished bussines sio nzuri kabisa kwahiyo kama kuna uwezekano fanya upate maelezo yake.Yanaweza yakaongeza uchungu kidogo ila mwisho wa siku ''KUJUA KWANINI'' kutakusaidia kukupa sababu ya wewe kujipandisha thamani kama unavyostahili na kuacha kumlilia mtu ambae hakukuthamini.Kitu kingine..ukijiskia kulia we lia tu wala usijikaze maana kulia kwa kiasi flani hua kunampa mtu ahueni.Cha muhimu uwe na mtu wako mmoja wa karibu akufariji now and then.Najua maana dada yangu aliwahi pata machungu ya mapenzi hivi hivi bila kujua kwanini mwenzake anaongea anayoongea basi ilikua ni kilio wiki nzima.Nikimbembeleza akatulia si muda mrefu ataanza kujiuliza kwanini kwanini na anaishia kulia upya.Ila kile kitendo cha kua na mimi pembeni kilimsaidia kuamua kwamba mtu asiyejali machozi yake kudondoka hastahili kuliliwa nae.

Mwisho jaribu kua na mawazo chanya wakati unasubiria maelezo yake.Inawezekana umeepushwa na baya zaidi....Inawezekana huyo sio wako uliyepangiwa kua nae.....Inawezekana hakujali wala kukuthamini sasa kwanini uumie juu yake......Inawezekana yote yaliyokufanya umpende sivyo alivyo...kama ana mitabia ya ajabu acha huyo dada mwingine akapambane nae.Kwa rehema za Mungu utampata atakaekupenda na kukuthamini kweli.Amua wewe kwamba it's probably for the best and you definately deserve better...AMINI NA ITAKUA!!
 
Wa kumpenda kwa moyo wako wote na akili zako zote na nguvu zako zooote ni Mungu tu.
Achana nae huyo jamaa. Move on!!
 
Pole sana mrembo, ndio dunia ilivyo. Na uzuri wa tatizo kama hilo likishakukuta ndio linakufanya uwe strong zaidi huko mbele ya safari. Hata hivyo ningependa kujua hili tatizo limekupata lini? yaani ni muda mfupi uliopita i.e last week au lina miezi? Manake si vizuri kuendelea kuumia kwa jambo kama hilo kwa muda mrefu sana, jifunze kusamehe ili maisha yaendelee.
 
Pole sana BJ....umeshauriwa vizuri na waliopita,mi nataka tu kukuambia Mungu anakupenda na amekuandalia mume,mpenzi mwingine....Time is a healer,huwezi yakwepa maumivu,kama ukijisikia kulia lia tu,yanapita na maisha yataendelea tu....kuna watu tulifikiri hatutawasahau kwenye maisha,lakini kwa sasa labda tukutane nao ndo tunawakumbuka......Just take a good care of yourself,love yourself even better,go out and cheer up, watch your beloved team MAN U,visit friends and above all pray....God will be with you through this....do not let this bring your confidence/self esteem down....you deserve the best and as long as you are still alive....the best is coming....May God God strengthern you....Keep shining!
 

Asha mamii, thanks in deed na umenipa faraja sana. Na pia nimeshindwa kuelezea hapa stori yote A-Z mana ilikuwa gumzo sana. Ingekuwa ni boyfriend tu ningejua hatuna committment zozote lakini baada ya mipango yote na mwisho wa 2011 nilijua tungekuwa wanandoa ila imegeuka sivyo.
Ishallah pumzi bado ninayo, ooh sweetheart yani nina machungu kweli especially kujua kitu too late!!


Pole dada BJ haya ndio maisha wewe ukipanga nae Mungu anakupangia, jitahidi kukubali hali hiyo na zidi kumuomba Mungu nae atakupa Mume mwema.

Asante mamii, kweli ni maisha tunapitia mengi..imeingia kwenye historia ya maisha yangu!..Nitatanguliza maombi zaidi!!


Pole BJ...
Unapotwa na matatizo ya kimahusiano, unazidi kuumia unapodhani labda wewe ndo tatizo la yeye kukuacha....
Hebu kubali tu kwamba hamkupaswa kuwa pamoja zaidi ya hapo mlipofika....and remember wewe sio tatizo....

Ni kweli hommie mana situation yenyewe ilivyotokea mpaka najiuliza mara 2-2..
Itabidi nikubaliane na hali mana sina cha kufanya zaidi ya kuikubali..Asante kwa ushauri RR,imenitia moyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…