Kumshitaki Mbunge Lusinde kwa matusi aliyomwaga Arumeru

Kumshitaki Mbunge Lusinde kwa matusi aliyomwaga Arumeru

Kiongozi, Sina shaka hata kidogo Lucinde asingekuwa bungeni angekuwa kibaka. Na kuna tofauti kubwa sana kati ya kauli za wana siasa na kauli za vibaka. Kauli alizotoa Arumeru, zinamfunua kabisa ukondoo wake, na kama Mtera waliamini wamemchagua mheshimiwa sasa wakae wakijua wapata kibaka. Hawana mbunge.

wapi william malecela? william, hama CCM haraka son, and you know what? the jimbo will be yours to lose!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa maneno haya nafikiri CCM wamefanya evaluation na wameona hata wakifanya kwa matusi hawana cha kupoteza, kwani mtu makini haweza kumpa mtu kutukana hadharani wakati anajua anashindana kutafuta kura na nataka kuamini huyo bwana alitumwa iliaje atukane.Na pengine wamegundua watanzania wakiambia matusi ndo wanatoa kura.
 
Kama anajibu mapigo inamaana mtu akimuuwa ndugu yake nae atamuuwa badala ya kulipeleka hilo suala kwenye vyombo vya sheria.

kwanini vicent hakupeleka swala la mkapa ktk ukoo wao ili litatuliwe na yeye kumpigia moja kwa moja

ndio maana nimesema kuwa hizo ndizo kampeni zinazoendelea huko arumeru,tatizo tu ktk hili la Lusinde limepata wasemaje ila lile la wasila kutoka kwa mdee halijapata wasemaje,hapo ndipo utaona utofauti

 
Last edited by a moderator:
quote_icon.png
By JacksonMichael
Ni kauli za kisiasa tu jamani, jadilini yalio na faida katika taifa lenu


Mkuu unashangaa nini wakati kila kukicha wapinzani wanaropoka mambo ya ajabu! sijaona cha kuwafanya mbowe a wenzake wapanic kwa kuwa ndio siasa za TZ kuattack personal kuliko sera.

Kilichonifurahisha hapa ni the way ulivyojibu.. Najua hata wewe muumini mzuri wa CCM yamekustua kiaci ambacho umejibu kwa unyonge sana.. Ndugu yangu kama viongozi wako wamekosea sio dhambi hata kidogo kuwakemea.. Alichokifanya Lucinde sio siasa.. Siasa haina matuci.. Kama wapinzani wanaropoka matuci haiwa-justify chama tawala nao watukane..!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ni kauli za kisiasa tu jamani, jadilini yalio na faida katika taifa lenu.

Mbona mmefungulia kesi kisa alisema Dr. Burian asipigiwe kura kwa sababu ni mwanamke tena hata hakufanya mabaya kama haya. JM unajua wazi Lusinde kawaharibia sana.
 
Nafikiri ukisikiliza vizuri utaona kila tusi alilokuwa akitoa alikuwa anatanguliza aliyoyasikia kwa chadema. Hii sasa kwangu imeniambia ni kwa nini miswada ya kijinga huwa inapitaga bungeni. Jamani huyu kaka sijui hapo anayeonekana kichaa ni nani??? ccm kuna watu naamini ni baba zangu kama wanatoa baraka kwa mtu kama huyu kutoa matusi akiwa ameeandaliwa mahususi tena mbele ya watoto, anastahili kuangaliwa ni aibu ya kudumu.

nashukuru sana mkuu kwa kunielewa

hayo ndiyo makosa ya kampeni za matusi kwa vyama vyote sio CDM wala sio CCM
 
Hapo hakuna kulea mashtaka ni lazima afunguliwe. Hili liko wazi na hata wakili mwanafunzi kesi hii anashinda. Kulea tabia hii ni hatari kwa taifa. Watoto utawakataza nini kama mjumbe wa halmashauri kuu hiyo ndo lugha yake. Hata CCM wenyewe kama wapo wachache wenye busara wanapaswa kuchukulia hatua za kinidhamu Lucinde.
Hii kanda itageuka mtaji mkubwa wa kuwachafua CCM kwa juhudi zao wenyewe.
 
Nimeona mulivyo biased nyinyi wachangiaji wote na ndiyo maana watu wanadai JF ni CDM. Wakati Mkapa anachafuliwa na mwendawazimu Vincent Nyerere muliona raha sasa CCM wameleta mwehu anayemzidi Vincent muna panic! Kweli mkuki kwa nguruwe....
 
Mimi naona hizi ni siasa tu za kawaida wala haina haja ya kumfungulia mashitaka!Kumbukeni kuwa hata mdee alimwita Wassira Sokwe hadharani hukohuko kwenye kampeni za Arumeru!!
 
Niitaka kusema kitu, lakini ngoja niache maana huyu Kilaza kajidhalilisha mwenyewe, team nzima ya campaign, chama chake, wapiga kura wake, serikari na wengine pia amefanya udhalilisha wa kijinsia. Sipati picha akina mama na akina dada waliokuwepo pale walivyo jisikia kwa matamshi yale. Huyu inabidi ashitakiwe na jamhuri.
 
Mkuu unashangaa nini wakati kila kukicha wapinzani wanaropoka mambo ya ajabu! sijaona cha kuwafanya mbowe a wenzake wapanic kwa kuwa ndio siasa za TZ kuattack personal kuliko sera.

Kuropoka mambo ya ajabu ni kuanika ufisadi ambao muda mwingi ulikuwa covered, sasa tuone maneno unayoona ya kawaida by Lusinde.
1. Mh Lema kaacha bwana, aliolewa mahabusu. (unajua mtu aliyeolewa hufanywa nini? Lusinde anaweza kuthibisha hilo?)
2. Mh Nyerere analiwa. (kwa lugha za vitarafa, neno kuliwa kwa alivotumia Lusinde ina maana a.na.la.wi.tiwa-aibu)
3. Mh Slaa anatembea kama kajinyea. Na ujinga mwingine mwingi alioongea utafikiri msukule au ndondocha.

Baya zaidi amuiga Idd Amin pale alipomwambia Mwl Nyerere (RIP) kuwa wapande ulingoni wapigane-aibu ccm.
 
Slaa, Lema, Mbowe, kumfungulia Lusinde Kesi ya Madai kwa udhalilishaji?



Tarehe 26.03.2012 katika eneo la Ngaresero, Usa River, Arusha, Lusinde, Mbunge wa Mtera, alitoa hotuba iliyolenga kuwadhalilisha baadhi ya viongozi wa chadema kwa hulka zao binafsi, inayolenga kuwachafua na kuwadhalilisha utu wao binafsi, na kauli ambazo kwa tafsiri ya wazi hazikuwa na tija kisiasa



Mh Lusinde alinukuliwa akisema


Lema (mbunge wa Arusha) .." alipata bwana magereza, "aliliwa", bwe*e, tunajua alifanywa nini"


Dk Slaa "alishindwa upadre na alifukuzwa kwa kutia mimba wanakwaya", "anatembea kama anajinyea", "ana mimba yetu" " anatishia kujamba wakati anaharisha" "kama dk slaa anataka fujo basi ianzie kwa mke wake" , "yule ngumi moja tu naua"


Mbowe – "ana uchungu wa mimba" "tumeshampiga mimba"
nassari – "(w)amepigwa mimba"


Kutokana na kauli hizi Lusinde yuko kwenye hatari ya kufunguliwa kesi ya madai na kufilisiwa kabisa.


Mtazamo ~ kauli hizi zinalenga kudhalilisha utu wa mtu binafsi na hazina mshiko wowote katika kukosoa sera za upande wa pili. Inawezekana kukosoa sera za wapinzani wako bila kuchafua utu, familia yake, au heshima yake mbele ya jamii. Kwa kweli hata kama kuna uhuru wa maoni, hii imepita kiasi. Kweli unajaribu kum -convince mpiga kura akupigie kura kwa kwa hoja ya "kupiga wanasiasa wenzako mimba" ? Sidhani kama hizi ndio sera za CCM. Lakini pia Lusinde alitoa kauli kuwa yeye "ni kichaa wa kuzaliwa" kwa hiyo inawezekana kweli hana akili timamu na CCM imeamua kumtoa kafara kichaa wao kwenda kulipuka na kutoa kauli ambazo yeye mwenyewe hajui madhara yake. Lakini pia ukifuatilia michango ya Lusinde Bungeti utagundua kuwa ukweli uwezo wake wa akili unatia shaka.

Baada ya uchaguzi kuna umuhimu wa huyu mtu kuchukuliwa hatua za kisheria angalau tujue uhuru wa speech unaazia na kuishia wapi, ili na sis wengine tukitaka kuropoka humu JF tujue madhara yake....



Video link //bofya hapa kusikiliza hotuba yake... Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru - YouTube

Hivi huyu jamaha ana elimu ya kiwango gani?c.c.m wanajichafulia sana,hii inatakiwa iwe ni criminal case na si civil,nimesoma gazeti la mwananchi la leo,baadhi ya wazee wa Arumeru wanasikitishwa sana na baadhi ya wanasiasa kupanda majukwaani na kutoa matusi badala ya sera!huyu Lusinde anawakilisha aina ya wabunge wengi wa c.c.m walivyo,hv huyu ni kiongozi wa wananchi kweli?hao wananchi waliomchagua wanajisiaje juu ya kuwakilishwa na mtu mbumbu kama huyu?cha kusikitisha eti kuna mwana jf nae ana support these rubbish kwa minajiri ya eti ni maneno ya kisiasa!wapi huo u great thinker wa wana Jf?huyo mtu ana tofauti gani na huyo Lusinde ktk uwezo wa kufikiri?maneno ya kisiasa kumchafulia mtu thamani ya utu wake kwa jamihi yote??what a shame!
 
Nadhani Lusinde atakuwa na matatizo ya akili akapimwe. Kwa kitendo alichofanya anatakiwa kushughulikiwa. Kama hizo ndo sera za ccm hatufiki. naona wameamua kuweka hadharani tabia zao sasa
 
Ni kauli za kisiasa tu jamani, jadilini yalio na faida katika taifa lenu.

Mkuu, umenisikitisha sana. Kweli wewe ni m-Tz halisi. Maana silka ya wa-Tz ni muache tu bwana, si kauchafua mdomo wake!!!!
Kweli? Mtu anatoa matusi machafu kiasi kile, tena mbele ya watoto, tena wengine ndiyo kwanza wametoka shule hata majumbani kwao hawajafika (wako na magegi ya shule) wakiwa na hamu ya kusikia sera za wakubwa na wanasiasa wanakutana na ahh......

Inatia kichefuchefu, ashughulikiwe kisheria ili liwe fundisho kwa wengine.
 
Kilichonifurahisha hapa ni the way ulivyojibu.. Najua hata wewe muumini mzuri wa CCM yamekustua kiaci ambacho umejibu kwa unyonge sana.. Ndugu yangu kama viongozi wako wamekosea sio dhambi hata kidogo kuwakemea.. Alichokifanya Lucinde sio siasa.. Siasa haina matuci.. Kama wapinzani wanaropoka matuci haiwa-justify chama tawala nao watukane..!

Achan naye huyo utapoteza muda wako.
 
Back
Top Bottom