Kiongozi, Sina shaka hata kidogo Lucinde asingekuwa bungeni angekuwa kibaka. Na kuna tofauti kubwa sana kati ya kauli za wana siasa na kauli za vibaka. Kauli alizotoa Arumeru, zinamfunua kabisa ukondoo wake, na kama Mtera waliamini wamemchagua mheshimiwa sasa wakae wakijua wapata kibaka. Hawana mbunge.
Kama anajibu mapigo inamaana mtu akimuuwa ndugu yake nae atamuuwa badala ya kulipeleka hilo suala kwenye vyombo vya sheria.
By JacksonMichael
Ni kauli za kisiasa tu jamani, jadilini yalio na faida katika taifa lenu
Mkuu unashangaa nini wakati kila kukicha wapinzani wanaropoka mambo ya ajabu! sijaona cha kuwafanya mbowe a wenzake wapanic kwa kuwa ndio siasa za TZ kuattack personal kuliko sera.
Anyway, nafurahi kuwa anajiita yeye ni KICHAA WA KUZALIWA.
Ni kauli za kisiasa tu jamani, jadilini yalio na faida katika taifa lenu.
Nafikiri ukisikiliza vizuri utaona kila tusi alilokuwa akitoa alikuwa anatanguliza aliyoyasikia kwa chadema. Hii sasa kwangu imeniambia ni kwa nini miswada ya kijinga huwa inapitaga bungeni. Jamani huyu kaka sijui hapo anayeonekana kichaa ni nani??? ccm kuna watu naamini ni baba zangu kama wanatoa baraka kwa mtu kama huyu kutoa matusi akiwa ameeandaliwa mahususi tena mbele ya watoto, anastahili kuangaliwa ni aibu ya kudumu.
Mkuu unashangaa nini wakati kila kukicha wapinzani wanaropoka mambo ya ajabu! sijaona cha kuwafanya mbowe a wenzake wapanic kwa kuwa ndio siasa za TZ kuattack personal kuliko sera.
Slaa, Lema, Mbowe, kumfungulia Lusinde Kesi ya Madai kwa udhalilishaji?
Tarehe 26.03.2012 katika eneo la Ngaresero, Usa River, Arusha, Lusinde, Mbunge wa Mtera, alitoa hotuba iliyolenga kuwadhalilisha baadhi ya viongozi wa chadema kwa hulka zao binafsi, inayolenga kuwachafua na kuwadhalilisha utu wao binafsi, na kauli ambazo kwa tafsiri ya wazi hazikuwa na tija kisiasa
Mh Lusinde alinukuliwa akisema
Lema (mbunge wa Arusha) .." alipata bwana magereza, "aliliwa", bwe*e, tunajua alifanywa nini"
Dk Slaa "alishindwa upadre na alifukuzwa kwa kutia mimba wanakwaya", "anatembea kama anajinyea", "ana mimba yetu" " anatishia kujamba wakati anaharisha" "kama dk slaa anataka fujo basi ianzie kwa mke wake" , "yule ngumi moja tu naua"
Mbowe "ana uchungu wa mimba" "tumeshampiga mimba"
nassari "(w)amepigwa mimba"
Kutokana na kauli hizi Lusinde yuko kwenye hatari ya kufunguliwa kesi ya madai na kufilisiwa kabisa.
Mtazamo ~ kauli hizi zinalenga kudhalilisha utu wa mtu binafsi na hazina mshiko wowote katika kukosoa sera za upande wa pili. Inawezekana kukosoa sera za wapinzani wako bila kuchafua utu, familia yake, au heshima yake mbele ya jamii. Kwa kweli hata kama kuna uhuru wa maoni, hii imepita kiasi. Kweli unajaribu kum -convince mpiga kura akupigie kura kwa kwa hoja ya "kupiga wanasiasa wenzako mimba" ? Sidhani kama hizi ndio sera za CCM. Lakini pia Lusinde alitoa kauli kuwa yeye "ni kichaa wa kuzaliwa" kwa hiyo inawezekana kweli hana akili timamu na CCM imeamua kumtoa kafara kichaa wao kwenda kulipuka na kutoa kauli ambazo yeye mwenyewe hajui madhara yake. Lakini pia ukifuatilia michango ya Lusinde Bungeti utagundua kuwa ukweli uwezo wake wa akili unatia shaka.
Baada ya uchaguzi kuna umuhimu wa huyu mtu kuchukuliwa hatua za kisheria angalau tujue uhuru wa speech unaazia na kuishia wapi, ili na sis wengine tukitaka kuropoka humu JF tujue madhara yake....
Video link //bofya hapa kusikiliza hotuba yake... Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru - YouTube
Ni kauli za kisiasa tu jamani, jadilini yalio na faida katika taifa lenu.
Ni kauli za kisiasa tu jamani, jadilini yalio na faida katika taifa lenu.
Kilichonifurahisha hapa ni the way ulivyojibu.. Najua hata wewe muumini mzuri wa CCM yamekustua kiaci ambacho umejibu kwa unyonge sana.. Ndugu yangu kama viongozi wako wamekosea sio dhambi hata kidogo kuwakemea.. Alichokifanya Lucinde sio siasa.. Siasa haina matuci.. Kama wapinzani wanaropoka matuci haiwa-justify chama tawala nao watukane..!